Mara zote waTanzania tumejisifia utulivu, amani umoja na upendo katika nchi yetu ya Demokrasia. Na tumekuwa na tabia ya kuficha baadhi ya maovu tunayoyatenda humu kwenye jamii yetu ili hii sifa njema isiharibike. Lakini kwa kweli kuna mambo ambayo yanakuwa too much na yanaudhi...na ajabu yake sasa ni kwamba mambo hayo yanaendelea kutendwa na viongozi wa jamii yetu wamekaa kimya kama vile kwa wao kuwajibika kutaharibu kitu flani! Hii inakera sana!!
Jana kulikuwa na habari kwamba wanafunzi "wakaidi" wa Kibasila Secondary School ya Dar es Salaam wamepambana na polisi baada ya kuamua kufunga barabara kwa kuwa mwenzao mmoja aligongwa na gari alipokuwa akitoka shule. Soma hapa. Sasa hapo ndipo hasira yangu inapoanzia. Watoto hawa hawa walilala barabarani mwaka jana kwa tatizo hili hili kwamba mwenzao mmoja aligongwa na gari hapo mbele ya shule na mkuu wa mkoa akaenda wakaongea na kukubaliana kwamba mahali pale patawekwa taa za kuongoza magari. Hadi linatokea tukio la jana hizo taa hazijawekwa na badala ya kusolve tatizo kwa kuweka taa mahali hapo ndio hao wanafunzi wakaitwa wakaidi na nguvu ya dola ikatumika dhidi yao. hata mtu asiye na akili atagundua kwamba hawa wanafunzi wanachodai ni haki yao na walipaswa kupigwa mabomu ya machozi ni mkuu wa mkoa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani.
Eneo lile limekuwa na ajali nyingi sana na ni karibu sana na kituo cha polisi, swali la kujiuliza ni kwa nini eneo lile haliwekwi taa za kuongoza magari?? Tatizo ni pesa au umeme?? au labda ni eneo maalum la kukamulia damu za waTanzania kwa ajili ya kafara ya Taifa???
Hivi mnategemea hawa wanafunzi mnaowapiga mabomu leo kwa sababu tu wanataka haki yao kesho mtawaambia waache ubinafsi wakiingia maofisini watawasikiliza?? Tunatengeneza Taifa la watu wenye uchungu na chuki kwa dola na uongozi kwa ujumla.
Ingekuwa ni taifa la watu makini nilitegemea kwamba mkuu wa mkoa wa Dar es salaam pamoja na viongozi wa kikosi cha usalama barabarani wakiongozwa na mkuu wao wangekwenda kuomba radhi kwa wanafunzi hawa majasiri na kuanza ujenzi wa taa za kuongozea magari eneo hili mara moja!!
Ninafahamu kwamba hawa wahusika hawasomi hii blog yetu lakini kama kuna mtu anawafahamu hebu uwafikishie ujumbe huu na uwaambie kwamba tumechoshwa na mambo yao ya ajabu wanayofanya. Na pia kuna siku hawa watanzania wanaowafanyia haya watachoka!!
Mungu ibariki na kuilinda Tanzania,
Poleni sana wanafunzi wa Kibasila Sec School na pia hongereni kwa kitendo cha ujasiri mlicho fanya!!
Picha ya Michuzi Blog.
-Kaka Gee.
3 comments:
Mh, inasikitisha sana. Hatua zichukuliwe..
Right on Gee.
Nimefurahishwa sana na ulivyozungumzia kwa ushungu na hasira tukio hili ambalo katika jamii ya wastaarabu ni jambo lisilofikirika kabisa.
Chombo cha dola kinawezaje kutumia nguvu dhidi ya raia wasiokuwa na silaha? walichofanya wao ni kutaka haki ya usalama wao, walipoona hakuna linalofanyika na wao kuishia kuishi kwa mashaka kila leo, ilibidi kufanya mgomo huo ambao kidemokrasia wanayo haki hiyo, hata ikiwa wanadai kuwa wanafunzi hao walifanya uharibifu fulani, bado kuwatawanya haikutakiwa kutumia silaha kama vile unapambana na wezi. Viongozi wenye hekima ya kuongoza watu wangeweza kutatua mgogoro huo kwa maongezi baina ya pande mbili hizo na hivyo kuepusha shari kubwa hivi.
Yaani wanapambana na wanafunzi kama wasiojua saikolojia ya watoto na wanafunzi? wanastahili kujifunza toka nchi nyingine namna ya kukabiliana na maandamano ya wanafunzi na si kufanya kila tukio la maandamano kuwa ni uwanja wao wa mazoezi na ku-test vifaa vyao.
Wrong approach and excessive use of power for no sensible reason at all. Shame on the police force team.
I have a dream... that one day Tanzania will be a true democratic state that Tanzanians will have freedom of expression!!
Asanteni wapendwa kwa kuchangia na kusikitika pamopja nami katika uozo huu unaoendelea katika serikali yetu. Nadhani inahitajika maombi zaidi!
Gee.
Post a Comment