Jamani hii picha nimeikuta kwa blogger SUMO ambaye yeye ameandika hivi; "Kifaa cha kisasa kikionyeshwa tayari kukabili watanganyika kipindi cha uchaguzi, tumejitahidi sana kuwekeza huko kama South miaka ya 70! Hilo mbele sijui lakuondolea Ice barabarani ama kukusanya waandamanaji?"
Mimi kama mTanzania nahisi hivi ni kama vitisho na havifai maana ni kama kutuonyesha kwamba serikali imejiandaa kwa fujo. Kwani kuna fujo yeyote iliyotangazwa??
Jana mnadhimu wa jeshi alipiga "biti" kuhusu fujo ambazo mimi sijaona umuhimu wa kutengeza hiyo tension kwa waTanzania. Nadhani kuna kamchezo kachafu kanataka kuchezwa...Mungu atulinde!!
Mungu ibariki Tanzania...naamini sitachukiwa kwa kusema ukweli!!
3 comments:
Naunga mkono SBP, sijaona sababu ya kuwatisha wananchi kwa kiwango hiki, labda iwe jeshi limekosa kazi na linatamani sana izuke fujo ili lionyeshe umwamba wake, kitu ambacho sicho. Sisi si wajinga kiasi hicho cha kuambiwa kaa kimya la sivyo nitakuchapa wakati tunachozungumzia ni cha msingi na madai yetu ni halali na tena ni haki yetu.
Mara nyingine vyombo vya habari na majeshi ya polisi ndivyo vimekuwa vyanzo vya chokochoko katika nchi ambazo zimepitia misukosuko na vita.
Wao wafanye kazi ya kudhibiti wabaribifu huko mitaani, waachane na kujibizana na Wanasiasa au kutumia maneno ya Wanasiasa na kwenda kuyajibia kwenye vyombo vya habari kwa vitisho.
Haifai!
Inasikitisha sana Subi. Moyo wangu unaniuma sana kwa kweli. Sioni dalili za fujo ila naona dalili za mchezo mchafu. Nimefurahi kwamba wagombea wengine wameona dalili ya huu mchezo mchafu na wameliongelea kwenye kampeni zao. Yaani inaonekana kwamba CCM ni chama cha maisha hapa Tanzania.
Tunahitaji mabadiliko!
Ila swali langu ni kwamba kwa nini CCM wameogopa sana???
NAsikitishwa sana zaidi yenu na vitisho na maneno hayo ya wakuu wa jeshi. Tulichosikia ni kwamba wataalamu wa Propaganda wa CCM wameliingilia jeshi na kuweza kulitumia kutekeleza azma yao ya kudidimiza Upinzani. Tusitishwe na hayo... "eople's ........" Ensn
Post a Comment