Tafuta/Search This Blog

Monday, November 19, 2012

Zawadi kutoka mkoa wa KAGERA!

Nimetumiwa zawadi kutoka Kagera, nimeona ni vyema na wewe ukaziona.

Kwanza  ni hii kitu. Sikuelewa ndani kuna nini maana hii packaging ilikuwa baab kubwa!
Nikaweka chini na kufungua taratiibu na mara... 

Ndani kulikuwa na mayai lukuki ya kuku wa kienyeji!! Huu ujuzi wa asili wa kufunga sha vitu niliupenda sana. Hapa wametumia majani/ nyazi na juu wamefungasha na jani la mgomba lililo kavu. Mayai yalisafiri kwa usalama sana na hakuna hata moja lililopasuka!!

Alafu na Senene! Mambo ya huko. na sasa ivi ndio msimu wake!!!

Nawashukuru sana ndugu zangu na marafiki zangu Wanyambo wa Karagwe mkoani Kagera, na hasa dada Regina Kajara na familia yake.

No comments: