This is a production house where you will meet talented young men producing Video and graphic designing! SBP ina wataalamu wafuatao: Enson Msuya - Video and imagery specialist, marketing. Godlove Lwendo - Graphic Designer. You can contact us by these numbers, +255 784 494906, +255 756 025428 We will be more than ready to serve you for any of the service you will need from us as we have described them thereup.
Tafuta/Search This Blog
Thursday, September 26, 2013
AUTO TREND WITH SAUDI YOUTH.
Two current automobile trends with youths in Saudi Arabi right now include a dangerous stunt known as “sidewall skiing” (driving on two wheels) and "stoning," in which cars are raised atop stacked piles of rocks and bricks.
Picha za Yahoo News
Rais Kagame aongeza sauti yake kwa wakosoaji wa ICC
Rais Paul Kagame wa Rwanda, leo ameongeza zauti yake kwa zile za viongozi wa Afrika ambao wameishutumu mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, kwa kuwalenga tu viongozi wa Afrika.
Katika hotuba yake kwenye mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jumanne mchana, Bwana Kagame amesema Waafrika waliunga mkono muafaka wa kimataifa wa kuhakikisha wahalifu wanawajibishwa, na kubuniwa kwa mfumo wa kimataifa wa sheria wa kukabiliana na uhalifu kama huo, wakiamini kuwa mfumo kama huo ungeendeleza amani na usalama ndani na baina ya nchi, na kuendeleza usawa wa uhuru wa nchi zote. Badala yake, Bwana Kagame amesema mahakama ya ICC imekiuka malengo hayo.
ICC imeonyesha upendeleo ulio dhahiri dhidi ya Waafrika, badala ya kuendeleza haki na amani. Imelegeza juhudi za maridhiano, na kutumiwa kuwadhalilisha Waafrika na viongozi wao, pamoja na kuhudumia haja za kisiasa za wenye nguvu. Hakuna mahali ambako dosari ya ICC imeonekana zaidi kuliko katika kesi inayoendelea ya viongozi wa Kenya. Watu wa Kenya wameonyesha hamu ya kuponya vidonda vya zamani, kuridhiana na kwenda mbele. Ndio maana waliwachagua viongozi wao wa sasa wanaojibu mashtaka.
Rais Kagame amesema juhudi za maridhiano ya kijamii na kuendelea zinatakiwa ziungwe mkono, pamoja na juhudi za taasisi za kitaifa kukabiliana na uhalifu, badala ya kudhoofisha juhudi za kuziimarisha taasisi hizo. Amelitaka Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama kulizingatia suala hilo na mengine yanayohusiana na sheria za kimataifa, ambayo tayari yamewasilishwa kwao, ili kudumisha haki, usawa wa kimataifa, kuunga mkono juhudi za maridhiano na kuheshimu utu wa Waafrika.
Habari kwa hisani ya Radio.un.org/sw
Monday, September 23, 2013
Zaidi ya watu 60 wauawa kwenye shambulizi la kigaidi nchini Kenya
Takriban watu 62 wameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 150 wakijeruhiwa baada ya watu waliojihami wanaokisiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Al shabaab kushambulia jumba moja lenye maduka mengi kwenye mji mkuu waKenyaNairobi. Zaidi ya watu 1000 waliokolewa kutoka kwenye jumba hilo la Westgate ambapo pia hadi sasa watu kadha wanakisiwa kushikiliwa na magaidi hao. Jason nyakundi na taarifa zaidi.
(RIPOTI YA JASON)
Kulingana na Shirika la msalaba mwekundu nchiniKenyani kuwa hadi sasa watu 62 wamethibitishwa kuuwa wengine zaidi ya 150 kujeruhiwa huku watu 69 hawajulikani waliko kufuatia shambulizihilola kigaidi ambalo limelitikiza taifa laKenyana kuushangaza ulimwengu kwa ujumla. Hawa ni baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye jumbahiloambao walifanikiwa kukimbia na haya ni yale walioyashuhudia
(SAUTI ZA WANANCHI)
Magaidi hao wanaokisiwwa kuwa wangambo la kundi la Al shabaaab kutokaSomaliawalilivamia jumba la Westgate mwendo wa saa tano asubuhi siku ya Jumamosi ambapo walianza kuwafyatulia watu waliokuwa kwenye shughuli zao risai kiholela . Jumbahilo lina zaidi aya maduka 80 na hutembelwa sanana watu walio na uwezo wa kifedha. Masaa machache baadaye rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye pia alimpoteza mpwa wake wakati wa uvamizi huo alilihutubia taifa akililaani shambulizi hilo.
(SAUTI YA KENYATTA)
Jumba hilo kwa sasa limezingirwa vikosi vya jeshi la Kenya wanaojaribu kuwaokoa watu ambao bado wanakisiwa kushikiliwa mateka na magaidi hao huku milio ya risasi ikisikika mara kwa mara kutoka kwa jumbahilona moshi mweusi nao mara nyingine ukionekana kutoka kwenye paa la jumbahilo.
Wakati hayo yakijiri mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC imemruhusu makamu wa raias wa Kenya William Ruto ambaye amekuwa mjini Hague tangu juma lililopita akihudhuria kusikilizwa kwa kesi inayomkabili kuhusiana na uhalifu wa kivita kurudi nyumbani kwa kipindi ya juma moja baada ya yeye kutoa ombi la kutaka kurudi nyumbani kushughulikia hali iliyo sasa nchini Kenya baada ya kutokea kwa shambulizi la kigaidi.
kwa hisani ya : Radio.un.org/sw
KENYA, We are praying for you!!!
Wapendwa wetu waKenya,
Tunafahamu ugumu wa hali mnayopitia wakati huu. Tunalia pamoja nanyi na kwa kweli kitu pekee tunaweza kukifanya wakati huu ni KUWAOMBEA. Tunawakumbuka sana katika maombi ili wakati huu upite na Mungu awatie nguvu za kuvumilia na kuwapunguzia ugumu na uzito wa majonzi haya.
Tunafahamu kwamba matendo kama haya yanadhihirisha UWOGA wa maadui zetu, na tunajua adui huyu mtamshinda kwa UMOJA wenu. Kwa hiyo pigeni moyo konde na umoja wenu na utaifa wenu uongezeke sana sasa maana wakati kama huu mnahitajiana zaidi.
Mungu awe nanyi daima!!
We are praying for you!
SBP.
Wednesday, September 18, 2013
Nissan NAVARA INAUZWA!
Thursday, September 12, 2013
Friday, September 6, 2013
Tanzania VS Rwanda.... SULUHU HII IWE YA KUDUMU.
Thursday, September 5, 2013
HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI (MNH) WAPATIWA MSAADA WA MAGODORO 50 KUTOKA NEEMA WOMENS POWER GROUP CHA JIJINI DAR ES SALAAM. MEYA WA ILALA JERRY SILAA ALIKUA MGENI RASMI.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ta Taifa Muhimbili Sr. Agnes Mtawa akitoa hotuba fupi pembeni ya mgeni rasmi Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala Ndg Jerry Silaa katika tafrija fupi ya kupokea magodoro 50 kutoka katika kikundi cha akina mama cha NEEMA WOMENS POWER katika ukumbi wa mikutano wa Muhimbili (Board Room) |
His Worship the Mayor Jerry Silaa, Akikabidhi Magodoro 50 kwa Kaimu mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kama msaada uliotolewa na kikundi cha wanawake kiitwacho NEEMA WOMENS POWER GROUP |
Subscribe to:
Posts (Atom)