Tafuta/Search This Blog

Thursday, September 5, 2013

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI (MNH) WAPATIWA MSAADA WA MAGODORO 50 KUTOKA NEEMA WOMENS POWER GROUP CHA JIJINI DAR ES SALAAM. MEYA WA ILALA JERRY SILAA ALIKUA MGENI RASMI.

Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ta Taifa Muhimbili Sr. Agnes Mtawa akitoa hotuba fupi pembeni ya mgeni rasmi Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala Ndg Jerry Silaa katika tafrija fupi ya kupokea magodoro 50 kutoka katika kikundi cha akina mama cha NEEMA WOMENS POWER katika ukumbi wa mikutano wa Muhimbili (Board Room)

Katibu wa kikundi Mama Dedes akisoma hotuba ya kikundi katika hafla ya kukabidhi msaada wa magodoro 50 katika hospitali ya Taifa Muhimbili. Alieleza mpango wa kikundi ni kutoa magodoro 3000 kusaidia wanawakw na watoto wanaolazwa katika hospitali za mkoa wa Dar es salaam. Aliwahimiza woote waliopata kadi za kuchangia wanakumbushwa kutoa michango yao ili kutimiza ahadi ya magodoro 3000 waliyoitoa. 


His Worship the Mayor Jerry Silaa, Akikabidhi Magodoro 50 kwa Kaimu mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kama msaada uliotolewa na kikundi cha wanawake kiitwacho NEEMA WOMENS POWER GROUP
Picha kwa hisani ya Blog ya Michuzi

No comments: