Mtafiti
wa tabia za wanadamu Viktor Frankil anatujengea uwezo kujifahamu kuwa
tunaweza kuyakabili mazingira kwa kutimiza wajibu wetu. Dhana ya wajibu
inatokana na neno la kingereza “responsibility” ni sawa na “response –
ability”. Tafsiri yake ni mwitikio wa ndani ya mtu kuonesha uwezo wake
kwa kuchukua hatua ya kubadili mazingira yake ili kupata matokeo
tarajali kwa ajili yake na jamii inayomzunguka. Tuendelee na sehemu ya
pili...
Ukitamka
wajibu na kutimiza majukumu jeshini, wanajeshi wanakuelewa vyema.
Mifumo ya taasisi za kijeshi huwa imefanikiwa “kuwatengeneza” watu
wanaotafuta suluhisho hata nyakati ngumu na zenye changamoto katika nchi
zao. Mtazamo wa kifikra kwa kila mwanajeshi huwa ni kushinda bila
kujali ukubwa wa jeshi la adui au changamoto ili mbele yake. Tukitoa
mfano kwa hapa nchini, unaweza kukumbuka nyakati za majanga kama vile
mafuriko na uharibifu wa madaraja, kazi hizi hupewa wanajeshi na mara
wakiingia kazini, suluhisho la muda mfupi hupatikana ili magari
yaendelee huku suluhisho la kurejesha daraja kama limekatika ikifanyika.
“Hakunaga”
kulaumu au kulalamika jeshini dhidi ya hali ngumu au mazingira magumu.
Bali kutimiza wajibu kwa kupingana dhidi ya hali isiyoridhisha kwa
kuiondoa na kufanya mazingira wezeshi yanayoifanya mipaka ya nchi iwe
salama au mahala wanapolinda amani panakuwa salama kuishi na kufanya
shughuli za uzalishaji ili kukuza uchumi wa mtu mmoja moja anaetimiza
wajibu wake na nchi nzima kwa ujumla.
Watanzania,
hatuna budi kuishi kama wapiganaji ili lengo ya kuyadhibiti mazingira
na kusimika aina ya maisha tunayoyataka kwa ajili yetu na vizazi
vijavyo. Tafiti kutoka kwa wataalamu wa tabia za wanadamu zinaonesha
kuwa, lawama na manung’uniko huondoa uwezo wa kuona fursa ya kutatua
matatizo. Mtu akifanikiwa kutatua matatizo yanayomzunguka, hufanyika
kuwa ni shujaa kwa familia, jamii yake hali kadhalika taifa lake. Na
jinsi tatizo linavyozidi kuwa kubwa, ndivyo, thamani ya mtu anaetatua
tatizo itakuwa mara suluhisho likipatikana na hali yake kimaisha au
jamii ikibadilika kutokana na jitihada zake.
Ukisoma
habari ya Daudi na Goliathi ambayo huzungumzwa na kuandikwa mara kwa
mara kwa falsafa mbalimbali kutegemeana na mkutadha inazungumzwa.
Mathalani, ikitokea hata timu ndogo ya mpira (underdog) inakabiliana na
timu kubwa (giant) zinapambana, uchambuzi mwingi hufananisha kama vita
ya Daudi na Goliathi.
Daudi amekua shujaa mpaka leo si tu kwa taifa lake Israel baada ya kumpiga Mfilisti Goliathi, aliekuwa shujaa wenye uzoefu wa vita. Daudi amekuwa mfano wa kuiga (role model) kwa watu mbalimbali kupitia mifumo mbalimbali ya mafunzo kufuatia hatua yake ya kuchukua hatua (taking initiative) ya kuamua kupigana na adui yake na taifa lake na kufanikiwa kuondoa fedheha kwa taifa lake . Daudi alileta suluhisho kwa jamii yake na mpaka leo kajijengea historia na kuacha alama (legacy)
Daudi amekua shujaa mpaka leo si tu kwa taifa lake Israel baada ya kumpiga Mfilisti Goliathi, aliekuwa shujaa wenye uzoefu wa vita. Daudi amekuwa mfano wa kuiga (role model) kwa watu mbalimbali kupitia mifumo mbalimbali ya mafunzo kufuatia hatua yake ya kuchukua hatua (taking initiative) ya kuamua kupigana na adui yake na taifa lake na kufanikiwa kuondoa fedheha kwa taifa lake . Daudi alileta suluhisho kwa jamii yake na mpaka leo kajijengea historia na kuacha alama (legacy)
Kuna
nyakati inasikitisha kusikia habari au kusoma kutoka vyanzo mbalimbali
vya habari hapa nchini na kukutana na habari za matatizo na huoni
muandishi akija na njia mbadala au mkakati wa kutatua tatizo au hali
ngumu jamii inapitia. Kitakwimu, asilimia kubwa ya vyumba vya habari
vimepoteza uweledi. Tulitegemea waandishi wa habari kuja na taarifa za
kuleta fikra mbadala kwa kuonesha namna kutatua matatizo yanayoizunguka
jamaii mbalimbali hapa nchini, kuna baadhi vinajikita kuonesha matatizo
na madhaifu ya huku na kule na kuwajaza Watanzania hofu. Kumbuka habari
mbaya kama haina taarifa za mbadala za suluhisho, huleta hofu badala ya
matumaini kwa wasomaji.
Kuna
taarifa wiki jana ziliandikwa kupitia magazeti kadhaa kuonesha kuwa
viwanda kadhaa vya maziwa na samaki vimefungwa kanda ya ziwa. Kuna
maswali mengi ya kujiuliza, je, Watanzania wameacha kunywa maziwa? Soko
la samaki wa Tanzania limeanguka huko ughaibuni? Kwanini kuna maziwa
kutoka Kenya, Uganda, Afrika Kusini na Uholanzi yanauzika sokoni? Nini
kimesababisha viwanda kufungwa? Nini kikifanyika viwanda hivyo vyaweza
kurejea na kuendelea na kazi. Sijaona wanahabari wakifanya “homework”
ili kuipa jamii majibu ya fursa ya kuzalisha chakula na kusindika ili
kuendelea kuuza ndani na nje ya nchi kutokana na ongezeko la watu
duniani.
A.R.
Bernard anasema kwa kila kisababishi kuna athari yake (to every cause
there is effect), kama hupendi athari au matokeo, una wajibu wa kubadili
kisababishi (if you do not like the effect, change the cause)
Rais
Magufuli alitoa ahadi kutoa fedha kwa wanahabari siku ya tarehe
4.Novemba kama wataanzisha kampuni. Je, kuna wanahabari wamepeleka
andiko lenye kuonesha tatizo na kuja na njia-mdadala ya kuondoa tatizo
hilo katika jamii? Au kuna kampuni limekuja na mpango-mkakati mbadala
kuongeza uzalishaji katika sekta ya mahindi ili kuwa na uhakika wa
chakula cha kutosha ili kudibiti ongezeko la bei ya unga wa sembe na
dona?
Na kama andiko limekataliwa, ni mara ngapi hatua zimefanyika ili kupigia debe wazo mbadala.
Nanukuu
falsafa ya sheria ya pili kani mwendo kutoka kwa Newton. “The rate of
change of momentum, is directly proportional to the force applied”.
Kiwango cha kubadilika kwa kani-mwendo ni uwiano sawa na nguvu
iliyotumika. Tunatumia nguvu kubwa kiasi gani kuandika kutatua matatizo
ya nchi hii ukiwa ni wajibu wetu sisi wazalendo wa nchi hii?
Itaendelea...
Fredrick Matuja