Tafuta/Search This Blog

Thursday, March 26, 2009

Hivi ndio tulivyo!!

Moyo wangu huwa unaniuma sana ninapoona kuna mtu anashindwa kuwajibika. Na huwa unaniuma zaidi ninapoona kwamba chombo kikubwa kama serikali au idara ya serikali pia inashindwa kuwajibika bila sababu ya maana.


Kwa nini marazote huwa tunakuwa tunatoa solutions ya matatizo yetu baada ya tatizo kuonekana? Jambo baya hata likionekana hakuna anayesema kitu hadi madhara yatokee kutokana na ubaya huo ndio utasikia kila mkubwa anataka apewe kipaza sauti na yeye asiskike kwamba alisema...KWA NINI? inatia hasira sana!!


Miezi miwili iliyopita kulitokea ajali mbaya sana katika daraja moja Arusha aliyo claim maisha ya waTanzania wenzetu. Daraja ni jembamba na hata kabla ya ajali magari yalikuwa yanapishana kwa shida kidogo, hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kuona hilo!
kwa bahati mbaya ikatokea ajali pale, kila mtu akaona kuwa madareva ni wazembe inabidi matuta yawekwe kuanzia mbali sana kutoka darajani. Amri ya matuta ikatekelezwa. Matuta lukuki yamewekwa na kama una gari kama la KINGO safari yako itaishia kwenye hayo matuta ambayo nadhani pia yalijengwa kwa hasira!
Sasa pamoja na matuta yote hayo lile daraja ambalo liliharibiwa kingo zake na ile ajali hadi leo hakuna anayesema litengenezwe. Kumbuka kwamba daraja hilo ni muhimu sana katika kuiunganisha Africa ya mashariki! Sasa mimi sijui tunategeshea ajali nyingine, tunasubiri miujiza, tunasubiri tena amri ya mkuu au kuna siri zaidi ya uwezo wangu wa kufikiria... SIJUI!
Najua sio rahisi watu wanaohusika wakaisoma hii habari lakini kwa kweli inanitia uchungu sana na hasa ni kwa sababu napita juu ya daraja hilo karibu kila siku tena marambili!!
MUNGU IBARIKI TANZANIA, TUONDOLEE UJINGA NA UTUSAIDIE KUWA NA MAWAZO ENDELEVU KWA AJILI YETU NA VIZAZI VIJAVYO!
Hii ni picha ya daraja hilo nilipokuwa napita hapo jana. Liko vile vile kama lilivyokuwa baada ya ajali.
-Godlove.

No comments: