Tafuta/Search This Blog

Thursday, November 18, 2010

BREAKING NEWS!!!!!!!

Wabunge wa chama cha upinzani cha CHADEMA, wameinuka na kutoka nje ya ukumbi wa bunge muda mfupi baada ya rais Jakaya Kikwete aliposimama ili kulihutubia bunge la 10.

Wabunge hao wakiongozwa na mkuu wa kambi ya upinzani bungeni ndg Freeman Mbowe waliinuka kimyakimya wakati rais alipoanza kusema neno la kwanza na hali hii iliinua kelele kutoka kwa wabunge wa chama tawala(CCM) ambao kwanza walianza kuzomea na baadae wakaanza kushangilia kwa kusema CCM CCM CCM.

Rais Jakaya Kikwete alionekana kama hajategemea jambo hilo na alikaa kimya kwa mshangao hadi wabunge hao walipomalizika kutoka. Spika Anna Makinda ilibidi kusimama na kuwaambia wabunge waliosalia kutulia na Rais akaanza tena kuhutubia.

Hotuba inaendelea sasa.

Wednesday, November 17, 2010

Facebook haikuanza leo jamani!

Labda ulidhani ni ya siku hizi sana, sasa hebu ona miaka 2000 iliyopita mawasiliano yalikuwa hivi...

Tuesday, November 16, 2010

Stanley Atema Chehe Atangaza Kuanza rasmi Mchakato wa kuaga ubachela

Naitwa Stanley A. Msami

Natangaza kuanza rasmi mchakato wa Kuoa. leo tar 14 Nov 2010


Akimweka Hadharani Mchumba wake Jenifa..Jamani Analipa HAlipiiiiiii?


Analipaaaaaaaaaaaa


Joseph Msami akimpongeza Shemeji/Wifi mtarajiwa (Alimpa zawadi ya Khanga)

Wamama wakimpongeza Mwali (Mwai kwa Kipare)



Wadau wa karibu waliokusanyika.
Haya Matumizi Mbadala hayo ya meno....








Pozi la kukubali kuolewa.


Full figure! Aibu kwa mbaaaaaaaaaaliiii


Mwai pamoja na Mama Mkubwa wa Stanley.



Wazamiaji hawakosagi...


Mwisho Mzee wa familia Mr. Mchome aliomba wadau wafanye Pledge ili kuanza mchakato Mzima wa Harusi. Watu tuliahidi vya kutosha. Natoa wito kwenu wadau kutoa Pledge ili kijana wetu apate jiko. Sio kwa ndugu na Marafiki tu, bali hata wewe.
Wasiliana hapa kutoa pledge 0716176843. Karibu kwa maandalizi.

CHADEMA CHAPEPEZA BENDERA CHINA

Mdau wa blog ya Shalom Broz Elifadhili Solomon Muysa akiwa China Shanghai, Huko aliwakuta wanachama wa Chama cha Demokrasia na MAendeleo CHADEMA.

Wednesday, November 10, 2010

Fananisha taarifa hizi mbili!

Nikisema tumelogwa nitakuwa nakosea?? Hebu angalia hizi taarifa mbili. Ya kwanza inatoka kwenye chombo chenye dhamana ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) na ya pili inatoka katika ubalozi wa Uingereza ambao ulihusishwa kwenye taarifa ya kwanza!!
**********************************************************************
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: UCHUNGUZI KUHUSU TUHUMA ZA RADA


Tunapenda kuujulisha umma kuwa uchunguzi na ushahidi uliokusanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Shirika la Upelelezi - SFO la Uingereza kuhusu tuhuma za Rushwa katika ununuzi wa Rada, umeshindwa kumhusisha Bw. Andrew Chenge katika tuhuma hizo.

TAKUKURU inawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa chombo hiki kwa kutoa taarifa za kuwafichua wale wote wanaojihusisha na Rushwa kwani jukumu hili ni la kila mmoja wetu.

Imetolewa na
Doreen J. Kapwani,
Afisa Uhusiano-TAKUKURU
Novemba 08 , 2010

S. L.P. 4865,
Dar Es Salaam.

Simu: 2150043-6/2150360 Nukushi: (022) 2150047 Barua pepe: dgeneral@pccb.go.tz Mtandao www.pccb.go.tz


**********************************************

PRESS RELEASE

10 November 2010

PCCB’S STATEMENT OF 8 NOVEMBER RELATING TO THE BAE/RADAR CASE
The British Government is aware of a statement made by the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) on 8 November 2010. At this stage the case relating to BAe and its dealings in Tanzania is yet to go to court in the UK. It is therefore not possible to draw conclusions either way relating to those who were interviewed in connection with the case.

NOTES FOR EDITORS:

On 5 February 2010, the Serious Fraud Office (SFO) announced that it had reached a settlement with BAe following an investigation into a defence contract with the Government of Tanzania.

Regarding Tanzania, BAe has admitted that it failed to keep reasonably accurate accounting records in relation to its activities here. BAe has said it will plead guilty to the aforementioned offence, and that it will pay a sum of £30 million by way of a penalty and also for reparation to Tanzania. A hearing in the crown court will determine the amount of the financial order (fine) with the balance to be made available as an ex-gratia payment to the people of Tanzania.

The plea agreement between BAE and the SFO brought to an end all outstanding investigations by the SFO. However, because the plea agreement has not yet been before the crown court in the UK, it is not possible to say at this stage whether the agreement will stand.

A crown court judge will determine whether the plea agreement between the SFO and BAE can be accepted. The hearing will start on 23 November.
*******************************************************************************
Nionavyo mimi:
Taarifa hii peke yake inapaswa kuwawajibisha viongozi wa juu wa TAKUKURU ambao inaonekana wazi kabisa kwamba ni taasisi inayoendeshwa kwa kufuata matakwa ya watu wachache wenye uwezo zaidi! Hii ni aibu kubwa sana kwa taifa ambalo tumekuwa tukiimba kwamba tuna amani na haki! Ninatamani sana watoe tamko na ikiwezekana wajipe moyo na KUJIUZULU kwa manufaa ya taifa!!
Na mwisho kabisa naomba ninukuu Biblia takatifu ambayo inasema, "HAKI HUINUA TAIFA, BALI DHAMBI NI AIBU KWA WATU WOTE"
Dhambi ni pamoja na Rushwa, Uongo. Ninadhani kuna haja kubwa zaidi ya kuwa na siku moja ya kumuomba Mungu toba ya taifa maana watu wachache wamekuwa kama miungu watu na kutuharibia kiasi hiki!
Mungu ibariki Tanzania!

Blandina na Tusiime!

Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa!!! Dada Blandina na kaka Tusiime hatimaye wafunga pingu za maisha na kuyaanza rasmi maisha ya ndoa siku ya jumamosi tarehe 6 Nov. Arusi yao ilifungwa katika kanisa la KKKT usharika wa mjini kati Arusha na kufuatiwa na sherehe ya ukweli katika ukumbi wa Triple A. Mapicha ndio haya!!

Tabasamu la matumaini kabla ya kuingia ukumbini!






Tusiime



Blandy.




Testing the muscles!!




Mambo ya keki!










Sasa hapa ni mambo ya ku dance kwa kwenda mbele!!



Kaka Gee akiserebuka na mama wa Blandina.




Kaka Gee na wife wakiwakilisha SBP ndani ya mjengo!
Familia nzima ya SBP inawatakia maisha mema sana ya ndoa marafiki zetu Tusiime na Blandina.

Monday, November 1, 2010

Jimbo la Arusha mjini sasa ni la CHADEMA!!

Hatimaye jimbo la Arusha mjini limechukuliwa na CHADEMA kutoka kwenye mikono ya CCM!! Mbunge mpya sasa atakuwa kaka Godbless Lema na amemuangusha aliyekuwa waziri wa serikali ya Kikwete Dr Batilda Burhani.

Na kwa mujibu wa TBC1 wameeleza kuwa ni habari ya kustusha sana kwa waziri wa kikwete kuanguka!!

Hongera sana Godbless Lema na hongera sana CHADEMA!!

Mungu ibariki Tanzania!

Katika picha hii ya mwaka jana mwishoni, Godbless Lema(kushoto) akiwa na kaka Gee!!

George na Emiliana wafunga pingu za Maisha

George and Emiliana
Pozi la Pamoja


George

Emiliana



Wapambe kibao



Pokea pete hii


Nathibitisha kua sisi ni Mume na Mke


Keki


Pozi la kutokea

Wapambe wa .dot com




Benz

Wazazi

Misosi

Maakuli



Muziki ulifunguliwa