Tafuta/Search This Blog

Wednesday, November 10, 2010

Fananisha taarifa hizi mbili!

Nikisema tumelogwa nitakuwa nakosea?? Hebu angalia hizi taarifa mbili. Ya kwanza inatoka kwenye chombo chenye dhamana ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) na ya pili inatoka katika ubalozi wa Uingereza ambao ulihusishwa kwenye taarifa ya kwanza!!
**********************************************************************
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: UCHUNGUZI KUHUSU TUHUMA ZA RADA


Tunapenda kuujulisha umma kuwa uchunguzi na ushahidi uliokusanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Shirika la Upelelezi - SFO la Uingereza kuhusu tuhuma za Rushwa katika ununuzi wa Rada, umeshindwa kumhusisha Bw. Andrew Chenge katika tuhuma hizo.

TAKUKURU inawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa chombo hiki kwa kutoa taarifa za kuwafichua wale wote wanaojihusisha na Rushwa kwani jukumu hili ni la kila mmoja wetu.

Imetolewa na
Doreen J. Kapwani,
Afisa Uhusiano-TAKUKURU
Novemba 08 , 2010

S. L.P. 4865,
Dar Es Salaam.

Simu: 2150043-6/2150360 Nukushi: (022) 2150047 Barua pepe: dgeneral@pccb.go.tz Mtandao www.pccb.go.tz


**********************************************

PRESS RELEASE

10 November 2010

PCCB’S STATEMENT OF 8 NOVEMBER RELATING TO THE BAE/RADAR CASE
The British Government is aware of a statement made by the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) on 8 November 2010. At this stage the case relating to BAe and its dealings in Tanzania is yet to go to court in the UK. It is therefore not possible to draw conclusions either way relating to those who were interviewed in connection with the case.

NOTES FOR EDITORS:

On 5 February 2010, the Serious Fraud Office (SFO) announced that it had reached a settlement with BAe following an investigation into a defence contract with the Government of Tanzania.

Regarding Tanzania, BAe has admitted that it failed to keep reasonably accurate accounting records in relation to its activities here. BAe has said it will plead guilty to the aforementioned offence, and that it will pay a sum of £30 million by way of a penalty and also for reparation to Tanzania. A hearing in the crown court will determine the amount of the financial order (fine) with the balance to be made available as an ex-gratia payment to the people of Tanzania.

The plea agreement between BAE and the SFO brought to an end all outstanding investigations by the SFO. However, because the plea agreement has not yet been before the crown court in the UK, it is not possible to say at this stage whether the agreement will stand.

A crown court judge will determine whether the plea agreement between the SFO and BAE can be accepted. The hearing will start on 23 November.
*******************************************************************************
Nionavyo mimi:
Taarifa hii peke yake inapaswa kuwawajibisha viongozi wa juu wa TAKUKURU ambao inaonekana wazi kabisa kwamba ni taasisi inayoendeshwa kwa kufuata matakwa ya watu wachache wenye uwezo zaidi! Hii ni aibu kubwa sana kwa taifa ambalo tumekuwa tukiimba kwamba tuna amani na haki! Ninatamani sana watoe tamko na ikiwezekana wajipe moyo na KUJIUZULU kwa manufaa ya taifa!!
Na mwisho kabisa naomba ninukuu Biblia takatifu ambayo inasema, "HAKI HUINUA TAIFA, BALI DHAMBI NI AIBU KWA WATU WOTE"
Dhambi ni pamoja na Rushwa, Uongo. Ninadhani kuna haja kubwa zaidi ya kuwa na siku moja ya kumuomba Mungu toba ya taifa maana watu wachache wamekuwa kama miungu watu na kutuharibia kiasi hiki!
Mungu ibariki Tanzania!

2 comments:

Anonymous said...

Safi sana naungana kabisa na ninyi shalom Broz. Nijitihada za kimaksudi kabisa za kulinda maslahi ya watu wachache ambao wananuka tayari kwa ufisadi! Ni aibu sana, aibu tupu. Kama kanisa la Mungu we need to engage in prayers and to act at some point in time. Tumelala sana.

Anonymous said...

Safi sana naungana kabisa na ninyi shalom Broz. Nijitihada za kimaksudi kabisa za kulinda maslahi ya watu wachache ambao wananuka tayari kwa ufisadi! Ni aibu sana, aibu tupu. Kama kanisa la Mungu we need to engage in prayers and to act at some point in time. Tumelala sana.