Wabunge wa chama cha upinzani cha CHADEMA, wameinuka na kutoka nje ya ukumbi wa bunge muda mfupi baada ya rais Jakaya Kikwete aliposimama ili kulihutubia bunge la 10.
Wabunge hao wakiongozwa na mkuu wa kambi ya upinzani bungeni ndg Freeman Mbowe waliinuka kimyakimya wakati rais alipoanza kusema neno la kwanza na hali hii iliinua kelele kutoka kwa wabunge wa chama tawala(CCM) ambao kwanza walianza kuzomea na baadae wakaanza kushangilia kwa kusema CCM CCM CCM.
Rais Jakaya Kikwete alionekana kama hajategemea jambo hilo na alikaa kimya kwa mshangao hadi wabunge hao walipomalizika kutoka. Spika Anna Makinda ilibidi kusimama na kuwaambia wabunge waliosalia kutulia na Rais akaanza tena kuhutubia.
Hotuba inaendelea sasa.
3 comments:
Hongera sana CHADEMA kwa kuwa na msimamo. Cha msingi ni kujua wanachokifanya,sheria wanaiju!! Hakuna sababu ya kuendelea kukaa kumsikiliza raisi ambaye wao hawajamkubali. Mungu ibariki Tanzania.
Mkereketwa!
Hongera sana CHADEMA kwa kuwa na msimamo. Cha msingi ni kujua wanachokifanya,sheria wanaiju!! Hakuna sababu ya kuendelea kukaa kumsikiliza raisi ambaye wao hawajamkubali. Mungu ibariki Tanzania.
Mkereketwa!
Mi naona hiyo haisaidii wako bungeni kuwawakilisha wananchi majimboni kwao nasio kuleta ubabe, hiyo hasira na chuki haitawasaidia hata kidogo, wametudisapoint sisi tuliokuwa tunawategemea.
Post a Comment