Tafuta/Search This Blog

Monday, November 1, 2010

Jimbo la Arusha mjini sasa ni la CHADEMA!!

Hatimaye jimbo la Arusha mjini limechukuliwa na CHADEMA kutoka kwenye mikono ya CCM!! Mbunge mpya sasa atakuwa kaka Godbless Lema na amemuangusha aliyekuwa waziri wa serikali ya Kikwete Dr Batilda Burhani.

Na kwa mujibu wa TBC1 wameeleza kuwa ni habari ya kustusha sana kwa waziri wa kikwete kuanguka!!

Hongera sana Godbless Lema na hongera sana CHADEMA!!

Mungu ibariki Tanzania!

Katika picha hii ya mwaka jana mwishoni, Godbless Lema(kushoto) akiwa na kaka Gee!!

No comments: