Tafuta/Search This Blog

Monday, March 30, 2009

Why you must change your socks REGULARLY...






You might kill innocent victims!

Do you think you have the worst job?





RIDHIKA!!

EASTER CONFERENCE APRIL 2009

A Historic Easter Conference in Springfield MO
Hosted by Pastors Charles and Catherine Abihudi
April 10th-11th
Location:Executive Conference Center910 West BattlefieldSpringfield MO 65807
Time:Friday 6pm-10pm
Saturday 8am-10pm

Registration Fee: $15 Per person includes snacks, lunch and dinner for Saturday
Great Singers and Inspirational Speakers
Special Session for youth and singles
Special prayer sessions for blessings on your life, studies, relationship, work etc
Healing for the sick

For More information please contact
Pastor Charles Abihudi (417-619-4951)
Mrs. Catherine Abihudi (417-423-0591)
Mrs. Pauline Kerns (417-234-4814)
Accommodations:
Please contact Quality Inn for group discounts
3330 E Battlefield Rd
Springfield MO 65804

Daniel 9:22"I have now come to give you wisdom and understanding" says the LORD

Please make Plans to attend as
YOU WILL NEVER BE THE SAME AGAIN

Thursday, March 26, 2009

Beautful Tanzania (2)

Beautiful Traffic police ingawa wana aibu sana ndio maana huwa wanajificha!!

Beautiful buses na wachuuzi wenye upendo!


Beautiful fresh food sold by beautiful Tanzanians!

Hivi ndio tulivyo!!

Moyo wangu huwa unaniuma sana ninapoona kuna mtu anashindwa kuwajibika. Na huwa unaniuma zaidi ninapoona kwamba chombo kikubwa kama serikali au idara ya serikali pia inashindwa kuwajibika bila sababu ya maana.


Kwa nini marazote huwa tunakuwa tunatoa solutions ya matatizo yetu baada ya tatizo kuonekana? Jambo baya hata likionekana hakuna anayesema kitu hadi madhara yatokee kutokana na ubaya huo ndio utasikia kila mkubwa anataka apewe kipaza sauti na yeye asiskike kwamba alisema...KWA NINI? inatia hasira sana!!


Miezi miwili iliyopita kulitokea ajali mbaya sana katika daraja moja Arusha aliyo claim maisha ya waTanzania wenzetu. Daraja ni jembamba na hata kabla ya ajali magari yalikuwa yanapishana kwa shida kidogo, hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kuona hilo!
kwa bahati mbaya ikatokea ajali pale, kila mtu akaona kuwa madareva ni wazembe inabidi matuta yawekwe kuanzia mbali sana kutoka darajani. Amri ya matuta ikatekelezwa. Matuta lukuki yamewekwa na kama una gari kama la KINGO safari yako itaishia kwenye hayo matuta ambayo nadhani pia yalijengwa kwa hasira!
Sasa pamoja na matuta yote hayo lile daraja ambalo liliharibiwa kingo zake na ile ajali hadi leo hakuna anayesema litengenezwe. Kumbuka kwamba daraja hilo ni muhimu sana katika kuiunganisha Africa ya mashariki! Sasa mimi sijui tunategeshea ajali nyingine, tunasubiri miujiza, tunasubiri tena amri ya mkuu au kuna siri zaidi ya uwezo wangu wa kufikiria... SIJUI!
Najua sio rahisi watu wanaohusika wakaisoma hii habari lakini kwa kweli inanitia uchungu sana na hasa ni kwa sababu napita juu ya daraja hilo karibu kila siku tena marambili!!
MUNGU IBARIKI TANZANIA, TUONDOLEE UJINGA NA UTUSAIDIE KUWA NA MAWAZO ENDELEVU KWA AJILI YETU NA VIZAZI VIJAVYO!
Hii ni picha ya daraja hilo nilipokuwa napita hapo jana. Liko vile vile kama lilivyokuwa baada ya ajali.
-Godlove.

Praise and Worship Evening!!

kaka Enson akiongoza kikosi cha kusifu!!


TangiJ, Manaseh

Kikundi cha praise and worship, TAG Kigogo kimeanzisha ibada za kusifu na kuabudu mara moja kwa mwezi jumapili jioni. Ibada ya kwanza ilikuwa tarehe 22/03. kwa kweli ilifana na kila mtu alitamani kuona hiyo ibada itakayofuata! Kama upo Dar unakaribishwa!!





KUSIFU KUNAWAPASA WANYOFU WA MOYO!!

UKAME!




Jamani kwani huu ni mwaka wa njaa?? Hebu ona maeneo yalivyokauka sehemu ambayo huwa kunakuwa greenish kipindi kama hiki miaka mingine!
Eee Mungu tuepushie balaa hili la njaa na ukame!!

Monday, March 23, 2009

World Meteorological Day!


Leo ni siku ya hali ya Hewa duniani. Mamlaka za Hali ya hewa duniani kote zinasheherekea siku hii kwa kuweka wazi shughuli wanazozifanya kwa wananchi.

Katika siku hii mimi binafasi ninapata nafasi ya kuwa kumbuka marafiki zangu na ndugu zangu wengi wanaofanya kazi katika mamlaka ya Hali ya Hewa hapa Tanzania(TMA). kwa kweli ninawapongeza kwa kazi nzuri ingawa ni ngumu na ninawatakia wakati mwema katika kazi yenu.

Big up to; Noel Sanga, Kulwa Mbwambo, Chubwa, Mpinda, Catherine Masele, Hazla Shaaban, Hassan Ame, Kijazi Justice, Nyenyema Nyandindi Danford, Mgalula, Pamela, Lufurano, Abel Nyamenda, Mzee Mpatwa, Mande, Mayunga, Msomba, Kwedilima, Kaluse Athumani, Judica Mushi duh naona nikiwataja wote nitaishia hapa leo.


Miss you guys!!


-Godlove.

Friday, March 20, 2009

Spread LOVE...


"Spread love everywhere you go:
First of all in your own home...let no one ever come to you without leaving better and happier.
Be the living expression of God's kindness;
kindness in your face,
kindness in your eyes,
kindness in your smile,
kindness in your warm greeting."

-Mother Theresa

Tuesday, March 17, 2009

Beautful Tanzania

Beautiful people





Beautiful mountains






Beautiful rivers. (Wami)




Beautiful Indian ocean.





Beautiful Hotels



Beautiful streets

Beautiful Traffic jams!
Traffic jam inasaidia sana umoja wetu maana tunapata muda wa kuwa pamoja kwa muda mrefu tukiwa njiani.
I love Tanzania with all my heart! Im proud Tanzanian!





















Tuesday, March 10, 2009

Tunaelekea wapi?

Wananchi wenye hasira pamoja na polisi wakimtoa nje mtuhumiwa!!

Rais mstaafu,Ally Hassan Mwinyi,leo alikumbwa na jambo ambalo hakuna aliyelitegemea. Mwinyi alikuwa akihutubia wakati wa sherehe za Maulidi zilizofanyikia Diamond Jubilee. Punde si punde akatokea jamaa na kumchapa kibao. Kwa mujibu wa watu walioshuhudia kitendo hicho,kibao kilikuwa cha kushtukiza kwani kila mtu alidhani kijana huyo alikuwa anakwenda kumsalimia Kaimu Mufti Sheikh Suleyman Gorogosi aliyekuwa pembeni ya Mzee Mwinyi. Wengine walidhani kijana ni fundi mitambo na hivyo alikuwa anakwenda kurekebisha kipaza sauti. Tofauti na mawazo ya wengi,kijana huyo aligeuza mkono ghafla na kumnasa kibao Mzee Mwinyi. Kijana huyo ambaye ametambulika kwa jina la Ibrahim Said ana umri wa miaka 26.
Kabla ya kitendo hicho,Mzee Mwinyi,kama ambavyo amekuwa akifanya mara kwa mara,alikuwa akiwaasa waliohudhuria baraza hilo la Maulid kuepukana na ngono zembe kitu ambacho kinachangia sana kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi.

Baada ya hapo jamaa alitolewa nje na walinzi wa Mzee Mwinyi wakisaidiana na waumini huku akipewa kichapo cha nguvu kama inavyoonekana pichani. Baada ya kutolewa nje kijana huyo, Mzee Mwinyi alisimama na kuwahakikishia waliokuwepo kwamba yupo fiti na shughuli inaweza kuendelea!

Pamoja na hayo maswali kadhaa yameshazuka kuhusu jamaa wa usalama. Walikuwa wapi? Na je nini kilipelekea kijana huyo kufanya alichokifanya? Ni maneno yaliyokuwemo kwenye hotuba ya Mzee Mwinyi? Je kijana ana matatizo ya akili? Pole sana Mzee Mwinyi.
Picha kwa hisani ya Dr.Faustine.
Habari na picha kutoka Bongo Celebrity.

Friday, March 6, 2009

SWALI!!


Hivi maaskari wa usalama barabani wapo kwa ajili ya kuwasaidia madereva na watumiaji wengine wa barabara au wapo kukusanya mapato ya serikali (na yao binafsi)?????


Mbona huwa wanakaa maeneo ya kujificha? Wanamtega nani? Please help me!!

Tuesday, March 3, 2009

UTUMWA! JAMANI HATA HAWA WANA DAMU(Blood)

Mh jamani hata kama ni Punda. Je ungekua wewe ungekubali?

UMLI(Umri) - Age

Hapa tunaona Age inavyoathiri urefu wa mikanda. Mwe!!!

Thank God For March!!


It is another month! God has taken us through february and we have all the reasons to thank him! He is Good, isnt he?
Lamentations 3: 22 The faithful love of the Lord never ends![b] His mercies never cease. 23 Great is his faithfulness; his mercies begin afresh each morning. 24 I say to myself, “The Lord is my inheritance; therefore, I will hope in him!”