Tafuta/Search This Blog

Friday, October 30, 2009

Watoto..




Nimekutana na watoto katika mapozi tofauti, nikayapenda. Kuna wakati watoto huwa serious na wasikivu sana na kuna wakati wao wa kucheza. Tuwape nafasi!!

Friday, October 23, 2009

Dar Express Nini tena?????

Mara zote nimekuwa nikitumia mabasi ya Dar Express kwa safari zangu za kaskazini- mashariki mwa Tanzania. Kwa kweli nimeitambua kampuni hii kama kampuni inayoongoza na yenye mabasi mazuri na ya kisasa. Kama wiki mbili au tatu zilizopita nilipokuwa nikitoka Arusha kuja Dar nilipanda mojawapo ya mabasi haya na kwa kweli lilikuwa limezeeka, nilisikia kuwa lilikuwa limeanzia safari yake huko Karatu. Jamani hebu Dar Express mjirekebishe ili tuendelee kuwaamini na kuwatumia katika safari zetu. Mimi sikufurahia kabisa uchakavu wa basi lile, nadhani inabidi tu lirudishwe kwenye yard yenu kama vipi mlitengeneze au mliuze ili msiharibu jina lenu zuri.

Seheme ya kuegemezea mkono.

Foronya za viti!!



SIDHANI KAMA NITACHUKIWA KWA KUSEMA UKWELI!!

Polisi JAMII!!


Kama ulikuwa hujaielewa hii dhana ya Polisi JAMII basi mimi nimeikuta wazi wazi mitaa ya Tanga!!

Monday, October 12, 2009

Simon na Joyce!! 10/10/2009

Bi Joyce akiingia ndani ya ukumbiMch Titus Mkama, Msajili wa ndoa ya Simon na Joyce
Kuna mtu kati yenu ananeno lolote ili ndoa hii isifungwe? HAKUNA!!!
Mnatoa nini?
Nakupokea wewe uwe Mume/Mke wangu halali niliyekuchagua
Cheti cha ndoa
Baraka za ndoa
Bwana na Bi Arusi wameungana, sasa ni mmoja. (1+1=1) Mwe!!!!
Kaka G alikuepo!Wazaa Chema (Bwana Arusi)
UWazaa Chema Bi ArusiPPicha hii inanikumbusha Mbaaaaaaaaaali zaidi. pale nilipoambiwa kuwa Mch Mkama nndiye alifungisha/alikua msajili wa ndoa ya Mr & Mrs Clement Mbaga. wazazi wa Simon Mmbaga.
Pozi la kuunganaPamoja na wazazi

Kama kawaida ndani ya ukumbi wa Amecia TEC Baraza la Maaskofu






Hatimaye yametimia! Simon na Joyce walisogea mbele ya madhabahu na ndoa yao kufungwa jumamosi ya tarehe 10 october 2009 katika kanisa la TAG Kigogo Mburahati. Simon ni Braza wetu lakini pia ni mdau mkubwa sana wa maendeleo ya SBP. SBP ilikuwa karibu sana na tukio hilo na hizi ni baadhi ya picha zilizopatikana katika siku hiyo!!

Thursday, October 8, 2009

I believe in miracles!!


Just for a laugh!!

It is my day!!

Tarehe 8 Oktoba ni siku ninayokumbuka kuingia kwangu katika dunia hii kwa mara ya kwanza kupitia kwa familia ya Rev&Mrs Lwendo. Ninakaribia miongo 3 sasa humu duniani na kwa kweli ninayo kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa upendo, rehema, wema na fadhili zake nyingi sana kwangu. Mungu amekuwa kila kitu kwangu ninamtegemea yeye na ninathubutu kusema kwamba kwa lolote au chochote nilichonacho hakuna jitihada yangu hata kidogo bali ni msaada tu wa Mungu. Watu wengi wamefanya jitihada za aina mbalimbali wakaishia kupoteza kabisa hata maisha yao lakini mimi Mungu amenikirimu sana, namrudishia yeye utukufu.

Namshukuru Mungu sana kwa wazazi wangu. Wao mara zote wamesimama na mimi kunitia moyo kunifariji, kunibariki kwa maneno yao na hata kunionya nilipokuwa nakwenda chaka!! Mungu awape uheri wa maisha marefu duniani.

Ndugu zangu na hasa Shalom Broz (Josh na Enson) i really feel so good to have you by my side! Love you so much. Esther, Fadhili, Elias nawapenda!!

Mattie you decorated my life! Need i say more??

My friends; Jimmy, Andrew,Asumpta,Naomi, Ida, Allan Mhiro you mean a lot to me!!

God bless all of you for being part of my life!!



Kaka Gee katika Kaunda suit pembeni ya mama pamoja na baba akiwa amemshika Josh na mwishoni dada Esther!!


Kaka Gee siku za mwanzoni nilipoanza kazi Dar es Salaam. looking young!!


Kazini KIA - August 2009.


Recent picture, last week at the place where i live in Arusha!!
Mshukuruni Mungu pamoja nami!!








Monday, October 5, 2009

Ebenezer wa Sahara

Jamani msishange ni wiki ya graduation s hii. Graduand mwingine huyu hapa. Anaitwa Ebenezer Sahara!!

Mkaka akijipongeza na soda bariidiii baada ya kutunukiwa.


Mama Sahara (kulia) pamoja na rafiki akimshukuru Mungu pamoja na kijana wake.

Hefsiba akimpa tafu kaka yake.


Mzamiaji wa sherehe kama kawaida ndani ya nyumba...


SBP inampongeza sana Ebenezer pamoja na familia ya Sahara kwa hatua hii na inakutakia mafanikio katika yote na hasa katika mitihani ya kidato cha nne inayoanza wiki hii.

Paschaline

Katika kutembea tembea SBP imekutana na mdogo wetu mwingine wa St Joseph Ngarenaro ambaye alikwa akishherekea mahafal;i yake siku ya jumamosi. Na haya ndio mambo ya taswira siku hiyo.

Form 4's

Mgani rasmi katika mahafali hayo mh. waziri mama Nagu akifuatilia kwa makini

Paschaline akipokea cheti chake!



mama na mwana, full kicheko!



Paschaline akipozi na wadogo zake ambapo mdogo wake anayemfuata ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza shuleni hapo. Inaonekana wazazi wake wako na imani sana na shule hii...

SBP inamtakia Paschaline baraka zote katika maisha na mafanikio makubwa katika mtihani ulio mbele yake.

Calvary Temple Development Complex!!


Mambo yanaendelea vyema kabisa na zege limeshamiminwa na hapa linawekewa maji ili kuliimarisha.
Huu ni msingi tu tena ni upande mmoja tu wa jengo. SBP ipo katika eneo la ujenzi na picha na taarifa zaidi zitaendelea kukujia hapahapa!!

Sunday, October 4, 2009

St. Joseph Ngarenaro Secondary School - Arusha.

Shule ya wasichana ya St Joseph Ngarenaro ni moja kati ya shule maarufu na mashuhuri hapa Arusha na Tanzania. Shule hii imetimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1984. Jumamosi ya tarehe 3 Oktoba ndio yalikuwa maadhimisho ya silver Jubilee hiyo pamoja na mahafali ya kidato cha nne. SBP ilipata nafasi ya kuhudhuria na hizi ni baadhi ya picha.