Tafuta/Search This Blog

Friday, October 23, 2009

Dar Express Nini tena?????

Mara zote nimekuwa nikitumia mabasi ya Dar Express kwa safari zangu za kaskazini- mashariki mwa Tanzania. Kwa kweli nimeitambua kampuni hii kama kampuni inayoongoza na yenye mabasi mazuri na ya kisasa. Kama wiki mbili au tatu zilizopita nilipokuwa nikitoka Arusha kuja Dar nilipanda mojawapo ya mabasi haya na kwa kweli lilikuwa limezeeka, nilisikia kuwa lilikuwa limeanzia safari yake huko Karatu. Jamani hebu Dar Express mjirekebishe ili tuendelee kuwaamini na kuwatumia katika safari zetu. Mimi sikufurahia kabisa uchakavu wa basi lile, nadhani inabidi tu lirudishwe kwenye yard yenu kama vipi mlitengeneze au mliuze ili msiharibu jina lenu zuri.

Seheme ya kuegemezea mkono.

Foronya za viti!!



SIDHANI KAMA NITACHUKIWA KWA KUSEMA UKWELI!!

No comments: