Tafuta/Search This Blog

Monday, May 24, 2010

Be careful!...you are in ARUSHA

Nitaonekana kama ninapenda sana kuwasakama viongozi wa jiji letu la Arusha kwa kuandika haya ninayoandika, lakini huu ndio ukweli kwamba hawa wenzetu wamejisahau sana kwamba wanatakiwa kutimiza wajibu wao! Nilipokuwa natembea mjini jana nilipiga picha hizi ili ndugu zangu muone na wao kama watapata nafasi ya kuangalia waone. Natamani sana kama siku moja kiongozi yeyote wa hili jiji letu atanitafuta ili nimwambie vile ninahasira. Jamani kama mnawafahamu hebu waambieni kwamba mimi ninawasakama huku!!

Hapa ni katika barabara ya sokoine karibu na Metropole. Hili lipo tangu alhamisi... Ila nimependa huu ubunifu wa kuweka miti!!







Sasa haya mashimoyaliyowazi ni mengi sana hapa Geneva yetu. Sijui ni kwa sababu wenzetu wanapita huku barabarani na magari kwa hiyo haya hayawahusu?? Haya yako wazi kwa enzi!! Kuna siku mzee moja alitumbukiza mguu humu ndani ya shimo kuteguka! Jamani sina la kusema ila kama unakuja Arusha uje umejiopanga la sivyo ziara yako itaishia kwenye mashimo ya jiji!!

1 comment:

Anonymous said...

Yeah......that thing z more than a just chaos........hate irresponsible personnel hawa wa Jiji......nasema acheni kuraraaa...