Tafuta/Search This Blog

Sunday, May 30, 2010

Sasa ni zamu ya Kaka Raphael

Yametimia!! Aliyekuwa mmoja kati ya mabachela wakubwa wa Compassion International Tanzania, makao makuu Arusha kaka Raphael joachim Lyela hatimaye ameoa!!! Amemuoa dada Angel. Arusi yao ilifungwa katika kanisa la EAGT Elerai Arusha na sherehe kufanyikia Lush Garden. SBP kama kawaida tulizamia kwenye mnuso huu uliofanyika jumamosi ya tarehe 29 May 2010. Mapicha ndio haya!
Kaka mkubwa akitoa utambulisho.
Shemeji naye akitambulisha wa kwao.
Aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe!!
Baba mzazi wa Raphael, kaka Joachim Lyela akiwa makini kwenye sherehe.
Kwenye mitambo alikuwepo Papaa Jojo Jose Mwakajila, fullu sebene!!
Uso wa matumaini!
Keki na ukataji wake.
Kama unavyoona...
Yaonesha ilikuwa tamu sana maana imefumbiwa macho kabisa.
Mkurugenzi mkuu wa compassion International Tanzania, ndg Mayala akitoa nasaha zake kwa vijana wake.
Baada ya nasaha alipewa zawadi ya keki.
Wafanyakazi wa CIT wakielekea kumpongeza mwenzao.
Raphael anapenda sana vijana na hapa vijana wa EAGT Elerai wakielekea kumpongeza kaka yao.
Waliosoma na Raphael Mzumbe wakiwa na zawadi yao. Inasemekana kwamba raphel alipokuwa chuoni alikuwa napenda sana miwa. Bila hiyana walimletea mzigo mzima wa miwa ili asiwe mpweke sana kwenye honeymoon.
Bwana arusi akiwa na muwa wake wa kuanzia honeymoon.
Msosi time.
SBP iliwakilishwa na kaka Gee, na hapa ni katika meza ya maakuli!!
Eating is a very serious business!!
Marafiki wa Bwana Arusi .

Bwana arusi akirudi sebene pamoja na marafiki zake wa karibu, Patrick Mosha, Nsangalufu na Andrew Msegu. Hii ni baada ya kula!! Unaanzia kushoto....
...Unamalizia kulia!!!
Kamati iliyofanikisha mambo yote ya siku hii. pongezi kwenu.


Waleeee....
SBP inawatakia maisha mema yenye baraka nyingi za Mungu na mpate watoto jamani wawili watatu tufurahi tena pamoja. SBP pia inawatumia salamu nyingi kaka Andrew Msegu wa CIT pamoja na kaka Nsangalufu wa KINAPA. Tunawasihi muinue macho yenu juuu mkayaone mavuno yako tayari!!! Amen!!

2 comments:

Anonymous said...

Kumbe Rapha kaoa!! Walipeneza kwa kweli.
Picha zimetoka vzr sana hongera kwa SBP

shalom broz productions said...

Asante.