Tafuta/Search This Blog

Thursday, November 19, 2009

Tafakari...

Arusha.


Nilipokuwa natoka Arusha kuja ofisini kwangu KIA juzi, jana na leo nimekuta kuna shughuli nyingi barabarani za kusafisha barabara, kupaka rangi zile alama ambazo zilikuwa zimefifia kama hizi za zebra crossing na ile mistari ya katikati ya barabarani lakini jambo lililo nichekesha ni pale nilipokuta mafundi wanaweka mchanga katikati ya yale matuta aina ya rasta eti kupunguza makali ya hayo matuta kwa ajili ya ugeni VIP uanaotarajiwa kuja hapa nchini leo jioni.


Sasa ndugu zangu mimi jambo linalonipa shida ni kwa nini haya mambo yanasubiri wageni?? Kwani sisi wenyeji hatuhitaji barabara nzuri. Tunatoa kodi za kila aina lakini hawafanyi mambo yanayostahili kuturidhisha. Hii ni sawa na familia inayoweka vitu vizuri kama vyombo vya chakula kabatini hadi siku wakija wageni ndio wanatoa vitumike, kila siku wao wanatumia vyombo vikuu kuu vya plastic!!


Hebu serikali na itafakari kuhusu hili na ifanye mambo mazuri kwa raia wake bila ya kusubiria wageni kwanza....


Tafakari....


Chukua hatua....

NB: Picha hapo juu haihusiani na habari hii.

No comments: