Nimekuwa nikijiuliza mara nyingi sana kuhusu uhusiano wa wanyakyusa na uimbaji huu wa kuweka mabiti!! Ukienda Mbeya au hata popote pale Tanzania na hasa kwaya za makanisa ya Moravian utakuta huu uimbaji. Inavutia sana na inafurahisha sana sasa naomba ndugu zangu wanyakyusa mniambie hii imetokana na nini na imetokea wapi?? kaka Massapa Mwakulila, Mpoki Bukuku akina Tuntufye na dada zangu akina Atu na Bupe hebu nipeni jibu tafadhali!!
Nilirekodi video hii kwenye ibada ya umoja wa makanisa hapa Arusha na hii ni kwaya ya Moravian Mwanama.
Haki zote zimehifadhiwa.
1 comment:
Godlove,
Moravian wameintargrate Christianity with our culture.Kwa hiyo it is mandatory kwa makanisa ya Moravian, kuwa na Kwaya ya wazee ambayo itakuwa inaimba Kitamaduni , na Kwaya ya vijana ambayo inaimba bila kufungwa na sheria ya utamaduni.
Pia inabidi usahihishe. Kanisa la Moravian si la Wanyakusa tu, limeejaa tele kule Rukwa , Tabora na Iringa. Hivyo Wafipa, Wanyamwezi, Wandali , Wasafa nk wamejaa tele kwenye haya Makanisa. Sasa hivi hata hapa Arusha linaenea sana.
Huyo Bwana anayepiga hayo "mabiti" anaitwa Seme, ni moja ya hazina kubwa ya wanakwaya hapa Arusha. Hata kwenye harusi yangu mwaka 1997, aliipamba vilivyo. Na isitoshe siku hiyo palikuwa na Kwaya ya Moravian ya wamasai : You can imagine the experience!
Karibu kwenye kwaya yetu
Atubonekisye Massapa Mwakulila
Post a Comment