Tafuta/Search This Blog

Monday, April 5, 2010

Siku ya Amani na Joyce

Ilikuwa ni tarehe 27 March wakati kwa mara nyingine tena kambi ya mabachela ilipopata pigo jingine la nguvu kwa kumpoteza kiungo muhimu katika kambi hiyo kaka Amani kisinza ambaye aliamua kumchukua jumla binti wa mzee Lyatuu dada Joyce. Arusi hiyo ya kukata na mapanga na mashoka ilifungwa katika kanisa la Calvary Temple Arusha na sherehe kufanyika katika ukumbi wa Flamingo, Sakina.

Zifuatazo ni baadhi ya picha katika tukio hilo muhimu kwa maisha ya vijana hawa.

Joyce na Amani Full white!!

Pamoja na mashahidi wao nje ya kanisa.

Flowers, kutoka kushoto, Witty, Linda na Mercy. Tabasamu za kufukuza shetani!

Mr & Mrs A. Kisinza matumaini kibao baada ya kusign contract sasa ni kusherehekea tu!!

Amani akiwatambulisha ndugu jamaa na marafiki waliokuja kumsindikiza.

Joyce pia akitambulisha upande wake.

Ze Kekizzz!!

mh haya!


Joyce akipkabidhi keki ukweni.





Ndugu wa Joyce


Ndugu wa Amani wakiongozwa na wachungaji Lameck na Elieshi Kisinza waliosimama kulia.




Kama kawaida SBP iliwakilishwa na mkuu wa kitengo cha wanandoa kaka Gee na hapa alikuwa akitoa mawaidha ya mwisho kabla ya hanemun kwa bwana arusi!!

SBP inawatakia Amani na Joyce maisha ya ndoa yenye furaha na amani tele (kama majina yao) na baraka za Mungu ziwafuate na kuwapata siku zote za maisha yao. Bila kusahau mambo ya watotozzz!!!!!



No comments: