Tafuta/Search This Blog

Wednesday, August 4, 2010

TAKUKURU!!

Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza sana kwa kusikika kuliko kipindi chochote tangu kuanzishwa kwenu!! Ninaamini kuna waTanzania wengi walikuwa hawawafahamu na walikuwa pia hawajawahi kuelewa vyema kazi zenu lakini sasa karibu kila mtu anawahamu including watoto wadogo! Tena najaribu kuhisi kwamba ina wezekana kuna watu watakuwa wanadhani labda "takukuru" ni kipengele flani cha mambo ya uchaguzi maana kipindi hiki TAKUKURU imesikika mara mia zaidi! Kwa kweli mimi na SBP tunawapongeza sana kwa kusikika!!

Sasa ninatamani mnijibu jambo moja tu ili niwe na moyo mweupe kabisa!! Kwani kazi yenu ni kuangalia rushwa za uchaguzi peke yake au kwa makini zaidi?? Mimi ninaona kama mmezidisha nguvu sasa ivi kuliko kipindi kikngine chochote. Mbona mabarabarani kuna rushwa za waziwazi tu, mahospitalini kibao achana na ofisi nyingine za kutolea huduma?? Mimi nadhani kama mmngekuwa na ksi hiyo mliyonayo kwenye uchaguzi mkaiapply kwenye mambo yute Tanzania ingekuwa ya kwanza Africa kwa kupambana na rushwa.

Nadhani kuna kitu cha kujifunza na kufanyia kazi! Maana sasa ivi mmezama kwenye uchaguzi kwingine mmesahau! Hebu prove yourselves right kwa kufanya vizuri au kama ikishindikana uchaguzi ukiisha mrudi kwa kasii, hatutawacheka!!

Habu libadilisheni hili taifa jamani.

Ninaamini sitachukiwa kwa kusema ukweli...

-Godlove.

1 comment:

Anonymous said...

Kaka Takukukuru inakamata wala Rushwa wadogo wadogo, wale wa Dowans je, wale wa Rada, wale wa EPA