Tafuta/Search This Blog

Thursday, September 30, 2010

More from Fadhili and Catherine's wedding day

Kwanza Catherine almuangalia mumewe....


Kisha akamkumbatia na kumbusu baada ya kula keki...


Wafanyakazi wenzake na Fadhili (VETA) wakiongozwa na mkurugenzi mkuu wao wakipiga picha ya ukumbusho baada ya kumpa kijana wao mkono wa pongezi.

Vuvuzela orojino kutoka kwenye wooza pia lilikuwepo kumtoa kijana wetu kimasomaso...

Najua ndugu zangu wenye apetite hapa mtapata shida sana....huu ndio msosi uliokuwa kwenye sahani yangu wakati wa huu mnuso mkubwa.
SBP inawatakia Fadhili na Catherine maisha mema ya ndoa na heri na fanaka!

Tuesday, September 28, 2010

Siku ya Elifadhili na Catherine



Hatimaye yule kijana aliyejulikana kama bachela sugu, AMEOA!! Elifadhili Solomon Msuya amejivutia ubavu wake tarehe 26 september hii katika kanisa la TAG Kigogo DSM.
Ndoa hiyo ilisajiliwa na mchungaji Huruma Nkone na SBP kama kawaida tulikuwepo kumtoa kijana wetu ambaye pia ni mdau mzazi wa SBP.
Mipicha ndio hii...

Pastor Nkone akitoa neno la ndoa.

Kwa makini wakimsikiliza Pastor. Bestman Francis Saliboko akisikiliza kwa umakini mkubwa.

Ndio yeye?? Fadhili akihakiki kama hajapigwa changa la macho.






Hapa ni kuwekana kifungo cha pete.




Catherine akimvisha pete mumewe.



Wachungaji na wamama wachungaji wakiwaombea vijana wao ili wawe na maisha mema ya ndoa. picha zaidi zitakujia baadae.

Baadae ilikua tamu kama hivi....

Tuesday, September 21, 2010

ARUSI YA ELIFADHILI HIYOOOOOOO.....

Sisi Shalom Broz Production tunapenda kutumia ukurasa huu Kuwakaribisha katika Arusi ya Ndugu yetu, Kaka yetu Elifadhili Jumapili tar 26 Sept 2010 Pale Kigogo TAG. Baadae ni CASA Complex Hall Karibu na Kwa Nyerere Msasani. SBP tutakua tukipiga picha zote Mnato na Mtembezi.
Imetolewa na Utawala
SBP.

Monday, September 13, 2010

Timothy na Asumpta wapata mtoto!!

Marafiki na wadau wakubwa wa blogu hii, dada Asumpta pamoja na mumewe Timothy hatimaye wamebarikiwa kupata mtoto wa kike!! Mungu amewabariki na mrembo ambaye wameamua kumuita ZOELINE! SBP Arusha ilipata nafasi ya kuwatembelea wadau hawa na kupata taswira zifuatazo!

Mama , baba na mtoto wao.

Kaka Gee na Mkewe wakimuadmire mtoto.

Asumpta na Timothy.
Hongereni sana Timothy na Asumpta, Mungu aendelee kuwazidisha siku zote!

Pricilla wa Jojo na Matilda


Mrembo aliyezaliwa katika nyumba ya watumishi wa Mungu Mr&Mrs Mwakajila ndio huyu sasa, anaitwa Pricilla. Hapa akiwa ameshikwa na mama yake.

Baba mtoto.

Sisi tunawapongeza sana na tunawaombea mumlee katika njia ya Kristo!!


Saturday, September 11, 2010

Mambo ya wanafunzi wa shule za kata Dar...

Sekondari Dar wazichapa kavukavu, polisi yashikilia 20

KITUO cha daladala Tuangoma Wilaya ya Temeke jana kiligeuka uwanja wa mapigano baada ya wanafunzi wa Shule tatu za Sekondari tofauti kuamua kuonyeshana umwamba wa kupigana hadi kuumizana.

Wanafunzi hao ambao ni wa vidato tofauti katika shule za Sekondari Mikwambe, Tuangoma, Makongo na Changanyikeni zote za Wilaya ya Temeke walifanya tukio hilo muda mfupi baada ya kupanda katika daladala za kuelekea Tuangoma wakitokea Mikwabe.

Filamu hiyo iliyodumu kwa saa kadhaa ilisababisha wanafunzi 14, kujeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Temeke kwa matibabu zaidi.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, (DCP) Suleiman Kova alisema, uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wanafunzi hao wana mgogoro wa muda mrefu unaotokana na masuala ya kimapenzi wakituhumiana kuchukuliana wasichana.
Kwa mujibu wa Kamanda Kova, ugomvi huo ulisababishwa na baadhi ya wanafunzi wa shule hizo tatu ambazo zipo karibu.

Alisema taarifa za awali zinaonyesha wanafunzi hao ni watukutu, watoro wa vipindi darasani na muda wote hushinda vichakani bila kuhudhuria vipindi.

Kova alisema ugomvi baina ya wanafunzi hao ulianza wakati wakiwa katika daladala wakitokea Mikwambe kuelekea Tunagoma na kwamba walianza kurushiana maneno na baada ya muda mfupi walianza kupigana.

Kova alisema wakati vurugu hizo zikiendelea mwalimu Mkuu wa Shule ya Tuangoma alitoa taarifa polisi na muda mfupi baadaye askari walifika katika eneo hilo na kufanikiwa kuwakamata wanafunzi 20 wanaosadikiwa kuwa chanzo cha vurugu hizo. Majina ya wanafunzi hao, yamehifadhiwa.



Alisema jeshi la polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikana na Ofisa Elimu wa Wilaya ya Temeke pamoja na viongozi wa shule hizo, wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na mgogoro huo.

-Mwananchi.

Kwa mtazamo wangu hii ni aibu kwamba watoto wetu wanakwenda shule na kuanza kupigana kwa ajili ya mapenzi. Hii ni moja ya sababu ya under performance ambayo inaonekana kwenye shule zetu. Aibu sana!! wa kulaumiwa ni wanafunzi wenyewe na labda na wazazi wao kwa kushindwa kuwajengea misingi mizuri!!

Friday, September 10, 2010

Kufika kwanza, usalama baadae...

Ndio kawaida yetu, sijui ni kutokana na malezi au vipi lakini suala la usalama wa mtu binafsi anataka aambiwe na mkuu wa polisi au hata mkuu wa wilaya!!

Arusha.

Tuesday, September 7, 2010

Better titles

Let's start honoring our colleagues/employees with better titles for their professionalism

1. Garden Boy should be called - Landscape Executive and Animal Nutritionist (sio kijana wa ng'ombe).

2. House Maid: Domestic Operations Specialist (sio Beki tatu..)



3. Typist: Printed Document Handler



4. Messenger: Regional Business Communications Conveyer

5. Window Cleaner: Transparent Wall Technician



6. Temporary Teacher: Associate Tutor (sio Voda fasta!)




7. Tea Boy: Refreshments Overseer

8. Garbage Collector: Public Sanitation Technician



9. Watchman: Area Theft Prevention and Surveillance Officer (ukshindwa sana sema 'Afande')




10. Thief: Wealth Redistribution Officer (sasa je?)

11. Cook: Food Technician and Preparation officer.






Post courtesy of MARAFIKI HURU.

Friday, September 3, 2010

Mpya kutoka kwetu


Wapendwa wetu tunawaletea tena design mpya ya Tshirt ambazo tume design na kuprint wenyewe. Kama utapenda tshirt hizi tafadhali wasiliana nasi kwa namba hizi; 0786055413, 0759598340 na 0756025428.
Barikiweni sana!