Tafuta/Search This Blog

Friday, December 16, 2011

African Music




Kati ya vitu ambavyo Mungu aliwakirimia waAfrica ni kipaji cha muziki. Watu katika mazingira magumu waliyomo lakini bado wanasauti nzuri sana za kuburudisha unapozisikia. wakati leo mataifa yaliyoendelea yanalia hali mbaya ya uchumi, sisi tumezaliwa katika hali mbaya ya uchumi lakini bado tuna kitu cha kuimba na kufurahi.

Msikilize Lokua Kanza na sauti tamu sana. Ni mmoja kati ya wanamuziki wa Africa ambao kila anachoimba ninaweza kusikiliza!

Mungu Ibariki Africa.

Monday, November 21, 2011

Kumbikumbi!

Msimu wa mvua huwa na neema hizi pia. Jirani yangu aliwakamata hawa chakula wengi akaniletea na mimi. Nilisahau kuwapiga picha hadi walipokuwa mekaribia kabisa kuisha nikaona tufaidi pamoja na wewe mdau. Haya karibu japo mmoja wa kuonja hata kwa macho tu...

Wednesday, November 16, 2011

Tunapenda sana KUDHAMINIWA!

Nilipokuwa naperuzi kwenye blogu ya blogger mkongwe wa hapa nchini kwetu leo nimekutana na habari ya ajabu sana kwamba kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia kwenye kinywaji chake cha Grand Malt IMEDHAMINI graduu ya Mkwawa university Iringa!!! What a news!!

Hii ni ajabu sana kwa kweli! Kwani Mkwawa inamilikiwa na nani?? Na hivi inaingia akilini kwa mtu kwamba chuo kimeshindwa kufanya graduu hadi kipate udhamini?? na je kwani uongozi wa chuo ulikuwa unajua kwamba kuna siku wanafunzi watahitimu??? Nimejiuliza mengi sana na kwa kweli nimeudhika!!!

Tunapenda udhamini sana waTanzania,
Tunadhaminiwa net za kujikinga na Malaria
Tunadhaminiwa matangazo ya kufunga seat belt kwa ajili ya usalama wetu wenyewe...
Tunadhaminiwa matangazo kuhusu mahusiano kwenye ndoa zetu...
Tunadhaminiwa...
Tunadhaminiwa...

Sitashangaa siku hotuba ya rais ikidhaminiwa na USAID au siku kesi ya mahakama ya mwanzo itadhaminiwa na VODACOM!!!

Habari hii inapatikana hapa

Tuesday, November 15, 2011

Tanzania is still so beautiful!!

As i was travelling from Dar es salaam to Mwanza through Morogoro,Dodoma,Singida and Shinyanga i just felt like thanking God for this beautiful country. It is beautiful for sure, we are blessed...
God's arranged rocks near Mwanza.



Sukuma's traditional house. The land is so fertile.

Giant rock at Singida region.


Manyoni - Singida road.

Usimwambie mtu...

Hili kitu bado lipo barabarani. Nililikuta Singida last week.

Friday, November 11, 2011

Hatimaye Enson....


Enson akiombewa baraka na wachungaji.



Enson na mkewe Rest.





Enson yupo karibu sana na watoto na hapa walikuja kumpongeza.


Uncle Temba akifuatilia kwa makini ibada ya ndoa iliyoongozwa na mchungaji Martin Pyuza kutoka TAG Muheza.






Mambo ya kekizz. Rest akimlisha mumewe huku kaka mkubwa Simon Mmbaga akishuhudia.




Mkurugenzi akipeleka keki kwa wakwe zake.



Familia ya mzee Solomon Msuya kwa pamoja wakiongozwa na mtoto mkubwa kaka David.







Wanandoa.


Mr&Mrs Mmbaga


Mr&Mrs Mwakisambwe.
Mr&Mrs Lwendo






Mkurugenzi hatimaye ameoa. Amemuoa Rest Kileo. Wote walisoma sekondari ya kilimo ya Ifakara, huko ndiko walipokutana. Arusi yao ilifungwa katika kanisa la TAG Kigogo Mburahati na sherehe kufanyika kwenye ukumbi wa Mwika, Sinza.

Thursday, October 20, 2011

Hatimaye Ghaddafi AKAMATWA!!!!

Habari zilizoandikwa hivi punde na BBC zinasema kwamba kiongozi wa Zamani wa Libya Kanali M. Gaddafi amekamatwa na kikosi kinachompinga.
Inasemekana amekamatwa akiwa na majeraha na amepelekwa kwenye hospitali kwa kutumia gari la kubeba wagonjwa.

Kwa habari zaidi fuatilia kwenye link ya BBC hapa chini.

UZINDUZI WA ALBUM YA MWANAHARAKATI WA HIP HOP GOSPEL, DOUGLAS PIUS. DPC TAR 16 OCTOBER 2011

DP akipaform wimbo unaoitwa hotuba. ulikuwa wa ukweli sana

Praise and worship team ya Boko basihaya ikiwa ina mtukuza mungu
huyu si mwanajeshi bali ni mwanamuziki, hapa anaimba wimbo unaoitwa MAJESHI MAJESHI


Saturday, October 15, 2011

Kumbukumbu ya Mwalimu JK Nyerere


Imetimia miaka 12, Tanzania bila mwalimu! Kama angekuwepo sijui angekuwa na maoni gani kuhsu taifa hili alilolipigania! Mimi na wewe hatujui, tunabakia kumkumbuka tu.

Kutoka mkuoani Mara SBP inakuletea taswira za hivi karibuni zinazohusu maisha ya baba wa Taifa letu.

Suti aliyovaa mwalimu mara ya mwisho alipokuwa anaondoka Tanzania kuelekea uingereza kwenye matibabu na ndio hakurudi tena.


Mwalimu wa mwalimu! Mzee huyu mwenye umri kama miaka 120 alimfundisha mwalimu JK Nyerere. Moyo wake umjaa malalamiko ikiwemo kunyimwa pension yake!

Mke wa mwalimu wa mwalimu.

Mnara wa kumbukumbu katika shule ya msingi ya Mwisenge aliposoma mwalimu.


Darasa alilosoma mwalimu.


Dawati alilotumia mwalimu katika shule ya msingi Mwisenge likiwa limejengewa ili kuhifadhiwa kwa ajili ya kumbukumbu.


Sehemu ya nyumba ya Mwalimu.

Gari alilotumia Mwalimu mara ya mwisho kabisa ya uhai wake likiwa katika eneo la makumbusho kijijini Mwitongo Butiama.


Ukipata nafasi unaweza kutembelea makumbusho ya mwalimu Nyerere huko Butiama na ukapata maelezo ya mambo mengi yanayomuhusu mwalimu kama raisi na pia kama baba na mwanakijiji. Kiingilio katika makumbusho hayo ni Tshs 1500 tu!

*********************************************************************************

Note, picha zetu leo tumeziweka alama kwa kuwa kumekuwa na watu wana tumia picha zetu kwenye blogs na magazetu bila hata ya kutuomba kibali au hata kuacknowledge! Kama utaipenda picha yetu please itumie na useme kwamba umeichukua kwetu kama ambavyo sisi mara zote hufanya!

Barikiweni!

Picha zote zimepigwa na Elias Msuya.

Wednesday, October 12, 2011

video - New life Band Live in Mwanza.

NEW LIFE BAND LIVE IN MWANZA


Jumapili ya tarehe 9October New Life Band walikuwa katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza kwa ajili ya tamasha la kusifu na kuabudu. Mambo yalikuwa mazuri sana na hizi ni baadhi ya picha!!
Eliud, Goodluck na Jimmy Kimutuo wakisebenesha!!
Kaka Abednego doing his things!

Jimmy, Abednego na mzee Gideon.
Pastor Isaya na Askofu Batenzi wakitoa neno la ufunguzi.


wananchi wakiserebuka - ayee Mungu wa milele wa mapendo Mungu wa milele!!

Saturday, September 10, 2011

Joseph Msami aamua kuachana na Ukapela amwoa Adelah Deo.

Joseph na AdelahKaribuni Ukumbini Joseph na Adelah


Kishumba orijino....

Misosi.






Joseph haamini kama amepata Jiko.




Adelah na Mchumba wa Enson.




Keki ya asili ilitumika katika Arusi hiyo. Keki ya Kipare, almaarufu, KISHUMBA.





Msami akiwa na Rest



Pozi la kuingilia Ukumbini.


Friday, September 9, 2011

SHAROBAROOO MEEEEEN

Pozi la Ki MR Bean


Kijana huyu, Frank Temba hujitambulisha kwa jina la Shabobaro na wakati mwingine Barobaro alipokembelewa na mpigapicha wetu chumbani kwake.