Tafuta/Search This Blog

Tuesday, July 28, 2009

Calvary Temple Development Complex!!

Kanisa letu la Calvary hapa Arusha lipo katika project kubwa sana ya ujenzi wa jengo jipya la kanisa. Project hiyo iliyoanza mwishoni mwa mwaka juzi hatimaye wiki hii msingi umeanza kuchimbwa. lakini kabla ya msingi ilibidi kwenda katika eneo la ujenzi na kuliweka wakfu kwa Bwana kwa kufanya maombi mahali hapo na kuombea hata udongo utakaobeba jengo hilo. Ibada hiyo ya kuluiombea jengo letu hilo ilifanyika jumapili iliyopita ya tarehe 26 Jul 2009. Hizi ni baadhi ya picha.


Rev. W .B Kimaro akisoma Neno la Mungu katika ibada hiyo.Eneo la ujenzi


Mzee wa kanisa, ndg Kiondo akichimba udongo katika eneo la ujenzi ili uwekwe wakfu na kufungulia rasmi kazi ya ujenzi wa Calvary temple Development Complex.


Mchungaji Wambura ambaye ni mhasibu mkuu wa TAG akiomba katika eneo la ujenzi.





Wazee wa kanisa wakiwa wamewakilisha washirika wote kwa kuushika udongo na kuuombea.




Vijana pia walikuwepo ambao ndio hasa watakao kuwa viongozi na washirika katika jengo hilo jipya. Kulia ni Victor wa Makere na kushoto ni Ivan.



Mshirika Tolla G.




Mshirika mwingine Robert Ngowi.




Maombi katika eneo la ujenzi.
kama ilifikiria hii project ndogo, hebu ona huu mchoro wa jengo hilo litakapo kamilika
*
*
5
*
4
*
3
*
2
*
1
*
*
*
0

That is CALVARY TEMPLE DEVELOPMENT COMPLEX!!

1 comment:

Anonymous said...

wow! nyc photos!!