Tafuta/Search This Blog

Thursday, April 29, 2010

Banda la Mambo ya Tume ya Nguvu za ATOMIC Tanzania Atomic Energy Commission

Nilivutiwa sana na maonesho katika Banda hili, hata nikaomba mwelimishaji anipige picha.
Wanashughulika sana na mionzi kama ilivyo ya Urani.

Athari za muda mfupi kwa atakyegusa mionzi kama ya Uraniam



Mwelimishaji aliniambia kuwa mpaka kuweza kutengeneza umeme hapa tanzania, inaweza kuchukua hata miaka kumi au zaidi. Hivyo tuna safari ndefu.

Teknolojia ya BlackMark Corporation

Blackmark nimewakuta katika Maonesho ya Vyuo vikuu, Hawa wanabidhaa kama N-Computing ambapo PC moja inaweza kuhudumia monita 6 kwa wakati mmoja na zote kufanya kazi kwa kujitegemea.
Wasiliana nao hapa BLock 46 Plot 718 Shekilango Road, Kijitonyama Dar es Salaam, Tanzania
Tel +255 22 2773938 +255715 400 719

Monitor hizi zimeunganishwa ktk CPU auComputer moja nakuwekewa huduma ya N computing.

Maonesho ya Vyuo vikuu Diamond Jubilee. Hapa ni Banda la SUA...

Banda la SUA. Sokoine University of Agriculture

Panya Weupe. Kwakweli kwa hali ya Kawaida ni wazuri, nilikua natamani hata niombe mmoja wa kufuga.


Panya huyo ni buku, na nimtaalamu wa kutegua mabomu. Ukileta bomu hapa lazima aamke.
Ktk banda hili nilipata nafasi ya kuuliza kwanini hawa panya hawakutumika kutegua mabomu mapema pale mbagala. ila waliletwa baadae sana. Mwelimishaji alisema hivi! Baada ya mabom kulipuka, haikua sawa kuwaleta wale panya ili kutafuta mabomu kwani anga lote mahali pale lilikua na harufu ya mabomu. Panya huyu angeshindwa aoneshe wapi.
Tembelea SUA ujionee.

Wednesday, April 28, 2010

Graduation Ceremony ya Mwanahamisi. TETCO

Mwanahamisi katika pozi la furaha ya Cheti cha Ualimu grade IIIA


Pozi pamoja na Bibi mpenzi

Mama akimvisha Shada, hii ni ishara ya Furaha na pongezi...


Chukua cheti, Umefanikiwa kuhitimu



Ninajua ninachokifanya. Nilikuja kusoma, sasa nahitimu.
**
**
**
Mwanahamisi ni mwanafuni wakwanza kitaaluma katika shule hii
kwa wasichana. Shalom Broz imefurahishwa na Utendaji wake
hata kumpa nafasi katika Blog yetu ili umma umwone binti
Shujaa kama huyu...
TETCO maarufu Tanga Elite ni Chuo binafsi Cha ualimu ambacho kimeanza hivi karibuni, Ni kizuri, mpeleke ndugu yako akasome..

Tanga Elite Teaching College (TETCO)

UtawalaMkurugenzi, Manager na Mrs Msuya

Wahitimu wakiimba

Mgeni rasmi katika mahafali. Afisa elimu Mkoa wa Tanga

Mwaka wa Kwanza.

Saturday, April 24, 2010

Tuesday, April 20, 2010

Picha zaidi ya picha... angalia kwa makini





Hizi ni baadhi ya picha ninazozipenda sana. ingawa imepigwa kawaida inaonesha picha nyingine za ziada. Inapendeza sana.

Monday, April 19, 2010

KUISHI KWA MATUMAINI


Kama unaishi kwenye nyumba yenye alama hii (X) lazima utakuwa na maisha ya mawazo sana.
Nimemkuta mkaazi huyu mitaa ya Moshi akiwa na mawazo sana...

Sunday, April 18, 2010

Maisha bora kwa kila mTanzania!

Huu ni mwaka wa uchaguzi (bila kujali utabiri wa sheikh Yahaya) na watawala wanakuja tena kwetu kutuomba kura/kula kama walivyokuja kwetu hapo awali.
Chama tawala katika kampeni za uchaguzi zilizopita walituahidi MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA. Hizi picha nimepiga kwenye weekend hii miaka mitano tangu maisha bora yalipoahidiwa...

Wamama wakiwa wanajikwamua kwa kuuza mbogamboga na matunda.


Haya ndio aina za masoko yetu.


Nyumba ya mTanzania.


Kijana wa kiTanzania akiwa anahesabu sarafu alizopata kwa kuuza vinywaji na biscuits.

Tuesday, April 13, 2010

Janeth's Kitchen Party...


















Haya ni baadhi tu ya mambo katika shamra shamra za kumkichenpatisha binti janeth, tukio lilifanyikia masaki barabara ya chole.



Saturday, April 10, 2010

Msosi msisimko!!


Lunch yangu jana!


Yaliyomo: Ugali, Dagaa, nyama ya kukaanga, spinach na parachichi. (pilipili kwa wiingiii)

Mbwa wa Arusha...

Jamani kama kila jiji litaamua kutengeneza bendera yake nadhani sasa jiji la Arusha kwenye bendera yake wataweka picha ya mbwa. Hakuna sehemu hawa viumbe wamezagaa kama katika hili jiji. Hivi mamlaka zinazohusika wanawaonaga kweli au ndio wamekaa kuvimbisha matumbo yao tu bila kufanya kazi?? Inakera inaudhi. Hawa niliwakuta nje ya Bank ya NBC, Arusha branch wanakula good time hawana wasiwasi tena ilikuwa ni mchana wa saa saba. Hii ni aibu kubwa sana kwa jiji hili mnaloliita Geneva ya Africa!!





Naamini sitachukiwa kwa kusema ukweli...

Wednesday, April 7, 2010

Daraja la mto Nduruma

Wengi wanaokaa Arusha na mikoa ya jirani wanalifahamu daraja hili linalopita juu ya mto Nduruma. Mahali hapa pametokea ajali nyingi sana na watu wengi wanasema mengi kuhusu eneo hili. Hii picha ni ya asubuhi ya leo nilipopita darajani hapo.

Tuesday, April 6, 2010

Kuna uhusiano gani kati ya uimbaji huu na Wanyakyusa??

Nimekuwa nikijiuliza mara nyingi sana kuhusu uhusiano wa wanyakyusa na uimbaji huu wa kuweka mabiti!! Ukienda Mbeya au hata popote pale Tanzania na hasa kwaya za makanisa ya Moravian utakuta huu uimbaji. Inavutia sana na inafurahisha sana sasa naomba ndugu zangu wanyakyusa mniambie hii imetokana na nini na imetokea wapi?? kaka Massapa Mwakulila, Mpoki Bukuku akina Tuntufye na dada zangu akina Atu na Bupe hebu nipeni jibu tafadhali!!

Nilirekodi video hii kwenye ibada ya umoja wa makanisa hapa Arusha na hii ni kwaya ya Moravian Mwanama.

Haki zote zimehifadhiwa.

Monday, April 5, 2010

Siku ya Amani na Joyce

Ilikuwa ni tarehe 27 March wakati kwa mara nyingine tena kambi ya mabachela ilipopata pigo jingine la nguvu kwa kumpoteza kiungo muhimu katika kambi hiyo kaka Amani kisinza ambaye aliamua kumchukua jumla binti wa mzee Lyatuu dada Joyce. Arusi hiyo ya kukata na mapanga na mashoka ilifungwa katika kanisa la Calvary Temple Arusha na sherehe kufanyika katika ukumbi wa Flamingo, Sakina.

Zifuatazo ni baadhi ya picha katika tukio hilo muhimu kwa maisha ya vijana hawa.

Joyce na Amani Full white!!

Pamoja na mashahidi wao nje ya kanisa.

Flowers, kutoka kushoto, Witty, Linda na Mercy. Tabasamu za kufukuza shetani!

Mr & Mrs A. Kisinza matumaini kibao baada ya kusign contract sasa ni kusherehekea tu!!

Amani akiwatambulisha ndugu jamaa na marafiki waliokuja kumsindikiza.

Joyce pia akitambulisha upande wake.

Ze Kekizzz!!

mh haya!


Joyce akipkabidhi keki ukweni.





Ndugu wa Joyce


Ndugu wa Amani wakiongozwa na wachungaji Lameck na Elieshi Kisinza waliosimama kulia.




Kama kawaida SBP iliwakilishwa na mkuu wa kitengo cha wanandoa kaka Gee na hapa alikuwa akitoa mawaidha ya mwisho kabla ya hanemun kwa bwana arusi!!

SBP inawatakia Amani na Joyce maisha ya ndoa yenye furaha na amani tele (kama majina yao) na baraka za Mungu ziwafuate na kuwapata siku zote za maisha yao. Bila kusahau mambo ya watotozzz!!!!!