This is a production house where you will meet talented young men producing Video and graphic designing! SBP ina wataalamu wafuatao: Enson Msuya - Video and imagery specialist, marketing. Godlove Lwendo - Graphic Designer. You can contact us by these numbers, +255 784 494906, +255 756 025428 We will be more than ready to serve you for any of the service you will need from us as we have described them thereup.
Tafuta/Search This Blog
Wednesday, October 30, 2013
Monday, October 28, 2013
KONGAMANO KUBWA LA UAMSHO NA MAOMBEZI
Hatimaye Papaa Samuel Sasali a.k.a the Blogger ameoa!
Mambo haya yasingekosekana asilani!! |
Ukweliii1 |
Hii picha muhimu sana! Nahisi Papaa alikuwa anamkabidhi rafiki yake Prosper Kijiti na kuweka msisitizo! |
Mr&Mrs Sasali wakisindikizwa na Mr&Mrs Mndeme. |
Picha zote zimetolewa Facebook page ya MC LUVANDA
Sunday, October 27, 2013
Sikiliza kuhusu daktari aliyejitolea maisha kuokoa wahanga wa ubakaji!
Denis Mukwege, daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kwa zaidi ya takribani miaka 15 amejitolea maisha yake kuokoa wahanga wa ubakaji huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC. Akihudumia kwenye hospitali ya Panzi huko Bukavu, hospitali aliyoianzisha mwaka 1993, Dkt. Mukwege na wenzake wametoa usaidizi wa kitabibu kwa maelfu ya wanawake waliokumbwa na wanaoendelea kukumbwa na madhila ya ubakaji. Katika makala hii, Joseph Msami alipata fursa kuzungumza na Dokta Mukwege ambaye alifika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa mazungumzo na Katibu Mkuu Ban Ki-Moon. Katika mazunguzo na Msami, Dokta Mukwege walijadili mengi ikiwemo alivyonusurika kuuawa mwaka mmoja uliopita.
Monday, October 21, 2013
MILIKI KIWANJA CHAKO POPOTE TANZANIA. KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM VIWANJA MAENEO YA KIGAMBONI, CHANIKA NK
UTAPATA ENEO LILILOPIMWA USIBUGHUDHIWE NA MTU YEYOTE. MAENEO NI MAKUBWA NA MSAADA WA KUPATA RIGHT OF OCCUPANCY UTATOLEWA KWA WATEJA WETU. |
TUNA HAKIKISHA VIPIMO |
Friday, October 18, 2013
JIWE KUU - Mwanza.
What a wonderful scene!! I have never seen a rock as big as this! |
Huu mjiwe ni balaa |
Eneo la Mihama linaonekana kwa chini. |
JIwe kuu! |
Mr &Mrs Lwendo above the JIwe kuu. |
Umeshawahi kusikia kuhusu Jiwe kuu?? Jiwe kuu ni mwamba mkubwa sana uliopo maeneo ya Bwiru Mwanza. Hili jiwe ni kubwa sana limetapakaa katika eneo kubwa lipo juu sana. Leo nilipata nafasi ya kutembelea huko na kuliona jiwe hili maarufu. Nadhani hii ni sababu nyingine ya hili jiji kuitwa Jiji la miamba. Kama serikali kupitia wizara ya utalii wangetumia fursa, hii nieneo jingine la ukweli sana. Shukrani Kwa GLTI.
Thursday, October 17, 2013
Taarifa ya habari ya radio UM-16th October 2013
Wapendwa, Tafadhali bofya link hapo chini kwa taarifa ya habari.
HABARI
Habari zaidi nenda Radio.un.org/sw
HABARI
Habari zaidi nenda Radio.un.org/sw
Tuesday, October 15, 2013
Mwalimu Nyerere miaka 14 baada ya kifo chake, fikra zake zazidi kuchanua
Julius Nyerere, Jabali wa Afrika- Mitizamo toka Arusha hadi Obama, kitabu kilichoandikwa kwa pamoja na Profesa Ali Mazrui na Profesa Linda Mhando. Je nini hasa lengo la kuandika kitabu hiki? Flora Nducha na Assumpta Massoi wa Radio ya Umoja wa Mataifa walipata fursa ya kuzungumza na Profesa Mazrui ambaye alikuwepo katika siku maalum ya kumuenzi Mwalimu Nyerere,mjini New York. Kwanza Profesa Mazrui anazungumzia kilichomtia hamasa
Monday, October 14, 2013
Saturday, October 12, 2013
Shindano la kimataifa la uchoraji picha kuhusu uokoaji sayari ya dunia.
Shindano hilo mahsusi kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 6 hadi 14, litafikia kilele mwakani ambapo ukomo wa kuwasilisha picha zilizochorwa ni tarehe 15 mwezi Machi mwaka 2014.
Wadau tunaomba muwahamasishe watoto kushiriki shindano hili na mshindi atapata zawadi ya $2000!!
Kupata maelezo zaidi tembelea Radio.un.org/sw
Wadau tunaomba muwahamasishe watoto kushiriki shindano hili na mshindi atapata zawadi ya $2000!!
Kupata maelezo zaidi tembelea Radio.un.org/sw
NYERERE KUENZIWA KWA TUKIO MAALUM JUMATATU 14TH OCTOBER, NEW YORK
Kwa mara ya kwanza Siku ya ya Baba wa Taifa la Tanzania,
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itaadhimishwa makao makuu ya Umoja wa
Mataifa tarehe 14 mwezi huu. Shughuli hii imeandaliwa na ubalozi wa Tanzania
katika Umoja wa Mataifa ambapo mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja
wa Mataifa Joseph Msami, amefanya mahojiano na Mwakilishi wa Tanzania wake
wa kudumu katika UM Balozi Tuvako Manongi na ameanza kwa
kumuuliza ninini umuhimu wa siku hiyo?
Shughuli hiyo itaenda sambamba na uzinduzi wa kitabu
kiitwacho JULIUS
NYERERE: Jabali wa Afrika katika medani za kimataifa
kilichohaririwa kwa pamoja na Profesa Ali Mazrui na Dokta Linda Mhando. Hayati
Mwalimu Nyerere alifariki dunia tarehe 14 Oktoba mwaka 1999 nchini Uingereza
kutokana na ugonjwa wa saratani ya damu.
Msami akimhoji balozi Manongi |
Friday, October 11, 2013
Taarifa za habari Kutoka Radio ya Umoja wa Mataifa.
Tunapenda kuwataarifu kwamba sasa tumejiunga na radio ya umoja wa mataifa idhaa ya kiswahili na hivyo taarifa za habari za radio hiyo zitakuwa zinapatikana hapa kila siku. tumeweka katika format/mfumo rahisi wa wewe kusikiliza bila tatizo lolote.
Endelea kuburudika na kuelimika kupitia Shalom Broz Productions.
Thursday, October 10, 2013
Nichague ipi??
Kuna vingamuzi lukuki hapa Tanzania sasa baada ya kuamua kuingia kwenye mfumo wa dijitali tukiachana na ule wa analojia. Kampuni za kutoa huduma hii zimekuwa nyingi sana na wote wanasema wao ndio bora na wenye picha nzuri zaidi. Sasa mimi nichukue ipi kati ya hizi au nisubirie AZAM TV maana nao nimesikia wako njiani wanakuja....Naombeni ushauri wenu wapendwa!
Wednesday, October 9, 2013
Monday, October 7, 2013
Friday, October 4, 2013
Thursday, October 3, 2013
JOYCE KIRIA / WANAWAKE LIVE WAFICHUA NDOA YA WATOTO!!
Najua kila mtu mwenye ufahamu wa kawaida kabisa atakuwa ameshtushwa sana na tukio hili. Yaani ni kama tuko nyuma sana na ninahisi tatizo kubwa ni umasikini na njaa za wazazi!
Tunampongeza sana Joyce Kiria pamoja na kipindi cha Wanawake Live kwa kufanikisha kufichua tukio hili. Dada Joy, Keep it up na Mungu akulinde maana maeneo mengine unayoingia ni hatari kama hili. Endelea kufichua haya majanga kwenye jamii zetu.
Video ni mali ya Wanawake Live/Joyce Kiria.
-SBP
Wednesday, October 2, 2013
TUMETIMIZA SEHEMU YA MALENGO YA MILENIA ,YALIYOSALIA TUNAPAMBANA - KIKWETE
maendeleo ya milenia umefanikiwa nchini mwake licha ya kwamba yako malengo
ambayo bado hayajafanikiwa matahalani usafi wa mazingira na kuanisha
mipango iliyopo katika kuyatimiza.
Katika mahojiano maaluma na Joseph Msami wa Idhaa ya Kiswahili ya radio ya
Umoja wa Mataifa Rais Kikwete amesema nchi zilizoendelea zimekuwa zikisita
kutimiza lengo namba nane linalowataka watoe asilimia saba ya pato la taifa
ambapo akitoa mfano kwa nchi kama Marekani amesema ni kiasi kikubwa na
hivyo kutotomizwa jamabo ambalo kwa ujumla linachelewesha utekelezaji wa
malengo hayo.
-Kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Radio Umoja wa Mataifa.
ambayo bado hayajafanikiwa matahalani usafi wa mazingira na kuanisha
mipango iliyopo katika kuyatimiza.
Katika mahojiano maaluma na Joseph Msami wa Idhaa ya Kiswahili ya radio ya
Umoja wa Mataifa Rais Kikwete amesema nchi zilizoendelea zimekuwa zikisita
kutimiza lengo namba nane linalowataka watoe asilimia saba ya pato la taifa
ambapo akitoa mfano kwa nchi kama Marekani amesema ni kiasi kikubwa na
hivyo kutotomizwa jamabo ambalo kwa ujumla linachelewesha utekelezaji wa
malengo hayo.
Kaka Joseph Msami akimhoji rais Kikwete. |
Subscribe to:
Posts (Atom)