Tafuta/Search This Blog

Wednesday, October 2, 2013

TUMETIMIZA SEHEMU YA MALENGO YA MILENIA ,YALIYOSALIA TUNAPAMBANA - KIKWETE

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete amesema kwa sehemu kubwa utekelezaji wa
maendeleo ya milenia umefanikiwa nchini mwake licha ya kwamba yako malengo
ambayo bado hayajafanikiwa matahalani usafi wa mazingira na kuanisha
mipango iliyopo katika kuyatimiza.

Katika mahojiano maaluma na Joseph Msami wa Idhaa ya Kiswahili ya radio ya
Umoja wa Mataifa Rais Kikwete amesema nchi zilizoendelea zimekuwa zikisita
kutimiza lengo namba nane linalowataka watoe asilimia saba ya pato la taifa
ambapo akitoa mfano kwa nchi kama Marekani amesema ni kiasi kikubwa na
hivyo kutotomizwa jamabo ambalo kwa ujumla linachelewesha utekelezaji wa
malengo hayo.

Kaka Joseph Msami akimhoji rais Kikwete.

-Kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Radio Umoja wa Mataifa.

No comments: