Tafuta/Search This Blog

Friday, August 28, 2009

Ze Kiingeredha hia endi zea

Kwa taarifa yako, Kiingereza ni JANGA LA KITAIFA likiwa ni janga linalofuatana kwa karibu sana na gonjwa la UKIMWI hapa Tanzania. Wengi wetu lugha hii imekuwa ngumu sana ikiwemo na mimi (ndio maana hata posts nyingi za blog hii zinakujia kwa kiswahili). Lkini jana nimeingia kwenye restaurant moja ya heshima sana nikakutana na MENYU ya kiingereza yani ikabidi tu nifanye ustarabu wa kuwashirikisheni wapendwa ili muone hali ilivyo tete.


Kama baada ya kuangalia picha hizi hujagundua tatizo fahamu kuwa na wewe ni muathirika na umechelewa kupata tiba! Pole.
Tupigie simu tukusaidie kama unajali maisha yako!!

No comments: