Tafuta/Search This Blog

Tuesday, October 28, 2008

ENSON HUYOOOOOOOOOOOOOOO

Hatimaye ile siku tuliyoiongelea saaana ya kuhitimu kwa mmoja kati ya wamiliki wa Shalom Broz Production ilifika na jum,amosi ilopita kaka yetu alikula nondo zake kuvaa joho hadharani. Amehitimu shahada ya Sheria (hata Sharia pia anaweza) katika mjengo wa Open University of Tanzania pale Kinondoni Dar es salaam.


hapa anaonekana kabisa kwamba haamini macho yake kwamba hatimaye amelivaa hilo joho baada ya kujipimia kwa karibu miaka mitano!!
Mama mdogo Shangwe akiwa na kijana wake, "Hongera mwanangu"
Usione kama kijana amerembua...jua kali hajazoea. Amezoea fullu kipupwe kwenye ofisi za SBP




Dada Erica akimvisha taji, duh mizawadi kibao yaani!! Kwa pembeni hapo kuna Bajaj ya ofisi. Najua wengi mlifikiria ni pikipiki ya polisi... yetu hiyo!! Kaka Solo kwa pembeni kiduuchu.



Mh.. Rafiki wa Enson Luckytrizzier....!!!! Pia alikuwepo!! Enson naye kwa aibu....!!!






Haya safari ya home sasa inaanza!! Sheria na Sharia ishachukuliwa...kazi inatafutwa. Kwenye hii picha tena inaonyesha jamaa anafaa sana kuwa Kadhi!!
Bodi ya wamiliki wa Shalom Broz Productions katika ofisi zoote yaani Arusha na Dar tuna mshukuru Mungu sana kwa ajili ya siku hii na tunawashukuru wooote waliofanikisha kwa namna yeyote ile kufikia siku hii. Shukrani za Pekee kwa familia zetu yaani familia ya Solomon Msuya, Muheza pamoja na familia ya Pastor Lwendo, Dar es salaam. Mungu awabariki sanaaa na kuwakumbuka katika yoote mtakayoweka mikono yenu kuyafanya.
Picha nyingine zitaendelea kuwajia!!



1 comment:

Anonymous said...

Hongera Enson Mwaya!! Well done. All the best katika kupata kazi.

Mattie.